MAJUKUMU YA IDARA NA VITENGO VYA OFISI

Majukumu ya Wizara yamegawika kulingana na muundo wake, kila Idara/Kitengo hufanya majukumu maalum iliyopangiwa kama ifuatavyo:

CHUO CHA UTAWALA WA UMMA

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

MAMLAKA YA KUZUIA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI ZANZIBAR

MAJUKUMU IDARA YA RASILIMALI WATU

 1. Kuratibu Mafunzo ya maendeleo ya Rasilimali Watu kwa Watumishi wa Umma.
 2. Kuratibu na kusimamia mpango wa miaka mitano (5) wa Rasilimali Watu na Mpango wa mwaka mmoja mmoja unaotokana na Mpango wa miaka mitano ya Rasilimali Watu
 3. Kufanya uhamisho wa Watumishi wa Umma
 4. Kutathmini na kutoa taarifa za kiufundi katika mfumo wa kielektoniki.
 5. Kutunza kumbukumbu za watumishi katika mfumo wa uwekaji wa kumbukumbu za Watumishi (Database).
 6. Kuratibu na kuandaa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa uwekaji wa kumbukumbu za watumishi.

MAJUKUMU YA IDARA YA MIUNDO YA TAASISI UTUMISHI NA MASLAHI YA WATUMISHI.

 1. Kuhakikisha Miundo Bora ya Mawizara na Taasisi inawekwa,
 2. Kuandaa Mifumo yenye kuleta ufanisi katika utoaji wa Huduma na
 3. Kufanya mapitio ya mara kwa mara kwa mujibu wa Sera na Sheria katika kutekeleza majukumu ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
 4. Kusimamia Maslahi ya Watumishi wa Umma,
 5. Kuimarisha na kuhuisha Miundo ya Utumishi kwa kuwapanga Watumishi katika Miundo ya Utumishi na Miundo ya mishahara kwa mujibu wa sifa na taratibu zilizopo.
 6. Kutoa Miongozo ya Miundo ya Utumishi, Miundo ya Taasisi na Miundo ya Mshahara
 7. Kutoa Miongozo na Matoleo yanayohusu Utumishi wa Umma.
 8. Kutoa Elimu ya uelewa na Ufafanuzi wa miongozo na Matoleo kuhusu masuala yanayohusu mishahara na mambo mbali mbali ya Utumishi wa Umma.
 9. Kuanzisha na Kusimamia matayarisho na utekelezaji wa Miundo ya Taasisi, Miundo ya Utumishi na Miundo ya mishahara na kufanya mapitio ya Miundo na majukumu kila inapobidi.
 10. Kushajihisha uanzishwaji na utekelezaji wa Upimaji Utendaji Kazi (Performance Appraisal System) katika Mawizara, Idara na Taasisi za Serikali na hatimae kufanya ufuatikliaji wa utekelezaji wake.
 11. Kutoa Muongozo wa Utayarishaji wa Uanzishwaji wa Mkataba wa Utoaji Huduma kwa Umma (Client Services Charter) na hatimae kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wake.
 12. Kutayarisha Miundo ya Utumishi (Scheme of Services) ma masuala mbali mbali yanayojitokeza kuhusu Utumishi wa Umma.

MAJUKUMU YA IDARA YA MIPANGO, SERA NA UTAFITI

 1. Kuandaa mpango wa mwaka na mpango mkakati wa maendeleo wa muda mrefu
 2. Kufuatilia, kukusanya na kuratibu mipango ya maendeleo ya Taasisi zilizopo chini ya Ofisi
 3. Kufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu mpango mkakati wa bajeti
 4. Kusiamamia mkakati wa mageuzi wa Sekta ya Sheria na Sekta ya Utumishi wa Umma
 5. Kutoa utaalamu na huduma kwa ajili ya maandalizi, kufanya mapitio, ufuatiliaji na tathmini wa Sera zinazohusiana na Ofisi
 6. Kufanya kazi Nyenginezo kama zitakazoelekezwa na uongozi wa Wizara kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Kazi

MAJUKUMU YA IDARA YA SERIKALI MTANDAO

 1. Kuaanda na kusimamia sera, kanuni na miongozo ya TEHAMA katika Utumishi wa Umma.
 2. Kuoanisha na kuratibu shughuli za serikali mtandao kwenye taasisi za umma kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.
 3. Kuendeleza mipango ya TEHAMA katika taasisi za umma kwa madhumuni ya kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa.
 4. Kuwawezesha watendaji wa Serikali katika matumizi ya TEHAMA ili kufikia hatua bora za utoaji huduma.
 5. Kuwezesha na kuratibu maendeleo na kukuza shughuli za utoaji huduma za Serikali kwa njia za kielektroniki na kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wananchi.
 6. Kutoa miongozo juu ya ununuzi wa vifaa vyote vya TEHAMA katika Utumishi wa Umma
 7. Kuhakikisha usalama wa TEHAMA katika Utumishi wa Umma unalindwa na kuhifadhiwa
 8. Kuweka vigezo vya utendaji pamoja na mfumo wa ufuatiliaji ambao utasaidia katika kupima matokeo ya maendeleo ya serikali mtandao kijamii na kiuchumi.
 9. Kutayarisha na kufanya kampeni ya kuinua uelewa wa wananchi juu ya huduma zinazotolewa kupitia Serikali Mtandao.
 10. Kutoa ripoti juu ya maendeleo ya utekelezaji wa Serikali Mtandao na mafanikio yake kwa Serikali na jamii kwa ujumla.

MAJUKUMU YA IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI

 1. Kutoa huduma za Uongozi wa Rasilimali Watu na Utawala kwa Wizara husika.
 2. Kusimamia Majukumu ya vitengo vilivyo chini ya Wizara.
 3. Kusimamia masuala ya Ajira, Mafunzo, kupandishwa vyeo kwa Wafanyakazi wa Wizara.
 4. Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yanayohusu watendaji.
 5. Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya Utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa matakwa ya sheria au maagizo maalum.
 6. Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (Ukimwi, Jinsia, Mabadiliko ya Hali ya nchi na mambo ya Idadi ya Watu).
 7. Kutoa huduma za kitaalamu na huduma za manunuzi na uhifadhi wa vifaa kwa ajili ya Idara nyengine.
 8. Kutoa huduma za Uhasibu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa kumbukumbu za hesabu, mapato na matumizi, ulipaji wa mishahara na matayarisho ya mafao ya uzeeni.
 9. Kuandaa na kusimamia mpango kazi wa Idara
 10. Kuandaa na kusimamia bajeti ya Idara.

MAJUKUMU YA IDARA YA UTAWALA BORA

 1. Kuimarisha na kukuza misingi ya utawala bora kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni nchini
 2. Kuziwezesha wizara, idara na taasisi za Serikali na Jumuiya za kiraia kufuata misingi ya utawala Bora
 3. Kuweka mifumo ya kupima viwango vya kuheshimu na kutekeleza misingi ya Utawala Bora katika ngazi zote
 4. Kuweka taratibu za kuimarisha uratibu na utekelezaji fanisi wa programu za Utawala Bora
 5. Kuhakikisha kwamba haki ya kupata habari inaheshimiwa vilivyo.
 6. Kuhakikisha kwamba tathmini ya uhakiki wa Utawala Bora inafanyika hapa Zanzibar.

MAJUKUMU YA OFISI KUU PEMBA

Kuratibu shughuli na kusimamia shughuli zote za Ofisi ya Rais-KSUUUB Pemba.

KITENGO CHA SHERIA

 1. Kuishauri Ofisi kwenye masuala ya sheria.
 2. Kupitia na kuandaa nyaraka za kisheria za Ofisi.
 3. Kupokea malalamiko na kuyashughulikia.
 4. Kuratibu masuala ya Sheria.
 5. Kutoa elimu ya sheria kwa umma.

KITENGO CHA TEHAMA

 1. Kuendeleza kutekeleza na masuala ya TEHAMA pamoja na Sera ya Serikali Mtandao (e-Government Policy) Wizarani
 2. Kuratib uwajishwaji na Uwendelezaji wa mkakati wa Mfumo wa Teknojia ya Habari na Mawasiliano
 3. Kushauri Uongozi wa Ofisi juu ya Matumizi Mazuri ya vifaa vya TEHAMA na PROGRAMU zake
 4. Kuratib maendeleo ya uhifadhi wa program katika kuhakikisha usalama wa Taarifa za ofisi
 5. Kuhakikisha kuwa vifaa vya TEHAMA na programu zake zinatunzwa ipasavyo
 6. Kuratibu na kutoa ushauri wa manunuzi ya vifaa na programu za TEHAMA
 7. Kuanzisha na kuratibu matumizi ya Mawasiliano ya kielekitroniki kwenye Local Area Network (LAN) na Wide Area Network (WAN)
 8. Kufanya utafiti na kushauri maeneo ambayo TEHAMA inaweza kutumika ili iwe chombo cha kuhuisha utoaji wa huduma Wizarani.

KITENGO CHA UGAVI NA UNUNUZI

 1. Kusimamia ununuzi wowote na uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni isipokuwa usuluhishi na kutunuku zabuni
 2. Kuratibu shughuli za Bodi ya Zabuni ya Wizara
 3. Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
 4. Kufanya kazi kama Sekritarieti ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
 5. Kuandaa mpango wa Ununuzi na Uuzaji wa mali za Wizara kwa njia ya Zabuni
 6. Kupendekeza ununuzi na uondoshaji wa mali za Wizara kwa utaratibu wa zabuni
 7. Kukagua na kuainisha upungufu wa mahitaji katika Wizara na kutoa tamko kuhusu mahitaji hayo
 8. Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili wazabuni kushiriki
 9. Kuandaa matangozo ya fursa za zabuni
 10. Kuandaa rasmu za Mikataba
 11. Kutoa mikataba iliyothibitishwa na kusainiwa
 12. Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mali za Wizara
 13. Kuandaa na kutunza orodha au kitabu cha mikataba yote ambayo Wizara imetunuku
 14. Kuandaa taarifa za kila mwezi kwa ajili ya Bodi ya Zabuni ya Wizara
 15. Kuandaa taarifa ya kila robo ya mwaka juu ya utekelezaji wa mpango wa ununuzi na kuwasilisha katika kikao cha menejimenti ya Wizara
 16. Kuratibu kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali katika Idara na vitengo vyote vya Wizara; na
 17. Kuandaa taarifa nyinginezo kadri zitakavyo hitajika muda wowote.
Close
Close