Kuhusu Wizara

Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeundwa baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 Machi, 2016 na inajukumu la kushughulikia sekta kuu mbili: Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kwa upande wa Utumishi wa Umma inajumuisha na taasisi sita Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Tume ya Utumishi wa Umma, Idara ya Habari na Teknolojia (Serikali Mtandao), Idara ya Mipango ya Rasilimali watu, Idara ya Miundo ya Taasisi, Utumishi na Maslahi ya Watumishi na Chuo cha Utawala wa Umma.

Kwa upande wa Utawala Bora, inajumuisha na taasisi nne, Idara ya Utawala Bora, Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Sekta mbili hizi zinaunganishwa na Idara zifuatazo: Idara ya Uendeshaji Utumishi, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti pamoja na Ofisi Kuu Pemba.

DIRA

Kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka utakaotoa huduma bora kwa jamii kwa kuzingatia misingi ya haki, sheria, demokrasia na utawala bora.

DHAMIRA

Kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii zenye ufanisi na tija kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu, sheria na utawala bora.

MAJUKUMU YA OR- UUUB

 1. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sera za Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
 2. Kuishauri Serikali kwenye masuala ya Utumishi wa umma na Utawala Bora.
 3. Kufanya tathmini ya rasilimali watu na kubainisha upungufu katika utumishi wa umma.
 4. Kutoa miongozo ya usimamizi wa utumishi wa umma.
 5. Kusimamia na kuratibu masuala ya uzingatiaji wa misingi ya utawala bora.
 6. Kuendeleza kujenga uwelewa kwa jamii juu ya masuala ya utumishi wa umma na utawala bora.
 7. Kusimamia masuala ya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za Serikali pamoja na matumizi ya rasilimali za umma.
 8. Kusimamia masuala ya matumizi ya Serikali mtandao.

TUNU/ MISINGI YA THAMANI

 1. Umoja katika utoaji wa huduma
 2. Kutokuwa na ubinafsi katika utoaji wa huduma,
 3. Uadillifu/ uamini
 4. Kuzingatia masuala ya jinsia
 5. Mashirikiano, uwajibikaji na uwazi
 6. Ufanisi na tija
 7. Huduma bora na kuwajalii wataka huduma
 8. Kuzingatia matokeo
 9. Thamani halisi ya pesa (value for money)
 10. Utunzaji wa siri

MUUNDO WA WIZARA

Ofisi ya Rais - Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaundwa na Taasisi zifuatazo:-

Close
Close