TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA KADA ZA SHERIA ZANZIBAR

Posted: 2022-09-13 14:47:03
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi ya AFISA SHERIA DARAJA LA II na KARANI SHERIA DARAJA LA III kama ifuatavyo:-

1.AFISA SHERIA DARAJA LA II: Katika Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo :-

1.Ofisi ya Rais, Ikulu - Unguja “Nafisi 1” na Pemba “Nafasi 1”
2.Afisi ya Mwanasheria Mkuu - “Nafasi 8”
3.Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka - “Nafasi 10”
4.Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma - “Nafasi 2”
5.Wizara ya Maji, Nishati na Madini- Pemba - “Nafasi 1”
6.Tume ya Utumishi Serikalini - “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka aroubaini na sita (46).
Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Asiwe muajiriwa wa Serikali.

2.KARANI WA SHERIA DARAJA LA III: Katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu.

Sifa za Waombaji:
Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiopungua miaka aroubaini na sita (46).
Awe amehitimu elimu ya Stashahada ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Asiwe muajiriwa wa Serikali.

Jinsi ya Kuomba:
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektronic wa maombi ya ajira (Zanajira) kupitia anuani ifuatayo:- http://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 14 Septemba, 2022 hadi tarehe 28 Septemba, 2022.

Mfumo huo pia unapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P. 1587,
ZANZIBAR. Muombaji anatakiwa kuanisha nafasi ya kazi aliyoombea

Kwa msaada wa kitalamu wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kupitia email: helpdesk@zanajira.go.tz au Simu Nam. 0773101012.

TANBIHI:
Tume ya Utumishi Serikalini inawatahadharisha waombaji wote kwamba ajira zinatolewa bure. Hivyo, wanatakiwa kujiepusha na Matapeli wanaotumia nafasi hizi kwa kujipatia kipato kisicho cha halali.
Close
Close