Makabidhiano ya Muundo wa Utumishi

news phpto

.

Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa umma Kubingwa Mashaka Simba amezitaka Taasisi za Serikali kuitumia na kuifanyia kazi miundo ya Utumishi inayotolewa ili kuweza kwenda sambamba na mabadiliko yaliyopo nchini .

Kauli hiyo ameitoa wakati akimkabidhi Muundo wa Utumishi Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Manunuzi na Uondoaji wa Mali za Umma hapo ofisini kwake mwanakwerekwe.

Amesema endapo miundo inayotolewa itasisimamiwa ipasavyo na kuifanyia kazi kwa haraka malalamiko kwa watumishi ya maslah yatapungua siku hadi siku.

Aidha amesisitiza inapopitishwa miundo ni vyema kuwajuulisha watumishi maeneo waliyopangiwa na madaraja yao ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa umakini unaotakiwa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Manunuzi na uondoaji wa mali za umma nd. Othman Juma Othman ameahidi miundo hiyo kuifanyia kazi ,na kuwapanga watumishi kwa mujibu wa kada zao.

Close
Close