Waziri Haroun Ali Suleiman Amesema muelekeo wa serikali upo katika kutatua migogoro kwa wawekezaji

news phpto

kutopka kitengo cha habari

Waziri wanchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman Amesema muelekeo wa serikali upo katika kutatua migogoro kwa wawekezaji , hivyo ni vyema kusuluhishwa kabla kufika mahakamani

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa utatuzi wa migogoro kwa wawekezaji huko katika ukumbi wa verde nje kidogo ya mji wa Z anzibar kwa niaba ya Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Ali Mwinyi

Amesema endapo migogoro hiyo itatuliwa mapema changamoto za wawekezaji zinaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka na maendeleo yake kuonekana na mabadiliko yanaweza kutokea .

Nae Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki ,Jaji Nestor Kayobena amesema mahkama ya Afrika Mashariki imepewa mamlaka ya kuweza kutatua migogomo ,bila ya kupitia Mahakamani ,kila nchi ikitaka kuendelea lazima kupatiwa ufumbuzi migogoro kabla ya kufika mahakamani na mabadiliko haya yatasaidia sana kwa zanzibar ,Tanzania na hata Afrika Mashariki .

Mapema Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt.Mwinyi Talib amesema Zanzibar imekamilisha rasimu ya sheria inayohusu njia mbadala za utatuzi wa migogoro .Vile vile amesema inatekeleza miradi mikubwa ya kibiashara ambayo inahusisha wawekezaji wakubwa

Pia amesema mkutano huo utasaidia utatuzi wa kibiashara na migogoro itakayojitokeza na kusaidia kuvutia wawekezaji.

Mkutano huo wa siku tano mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo njia bora za kutatua migogoro,uwiano wa utatuzi wa migogoro baina ya china na afrika pamoja mitazamo ya jumuiya katika utatuzi wa migogoro.

Close
Close