TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA NA SHIRIKA LA HUDUMA ZA MAKTABA

Posted: 2019-10-11 14:39:51
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi ya kazi katika Wizara ya Katiba na Sheria kama ifuatavyo:-

1. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

Aidha, Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Shirika la Huduma za Maktaba kama ifuatavyo:-

1. Mwangalizi wa Ofisi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utawala wa Umma au Rasilimali Watu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Mlinzi Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Mafunzo ya Ulinzi kutoka JKU au JKT.

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 18 Oktoba, 2019 wakati wa saa za kazi.
Close
Close