Govt. Logo

OFISI YA RAIS - UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

Govt. Logo

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA OFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS

Posted: 2020-02-10 15:22:28
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kama ifuatavyo:-

1.Taarishi Daraja la III “Nafasi 1” – Unguja

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kufaulu.

2.Dereva Daraja la III “Nafasi 1” - Dar es Salaam

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva na leseni hai ya udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3.Mhudumu Daraja la III “Nafasi 1” – Dar es Salaam

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 14 Februari, 2020 wakati wa saa za kazi

Contacts

Main Office
P.O.Box 3356
Zanzibar, Tanzania
Tel.: +255 024 2230038
Fax: +255 024 2230027
Mobile: +255 77 000000
Pemba Office
P.O.Box 112
Chake chake, Pemba
Tel.: +255 024 2452294
Fax: +255 024 2452291

Us

Home About Us Departments

External Links

IPA OCAG ZAECA