Govt. Logo

OFISI YA RAIS - UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

Govt. Logo

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KATIKA OFISI YA BARAZA LA MAPINDUZI ZANZIBAR

Posted: 2020-02-21 15:00:23
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar kama ifuatavyo:-

1.Afisa Ufuatiliaji na Tathmini Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi au Mipango au Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar2.Dereva Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
• Awe na leseni hai ya udereva iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


3. Uhudumu Daraja la III “Nafasi 3”


Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.


4. Msaidizi Afisa Tehama Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Habari na Mawasiliano (ICT) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar..


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 28 Februari, 2020 wakati wa saa za kazi.

Contacts

Main Office
P.O.Box 3356
Zanzibar, Tanzania
Tel.: +255 024 2230038
Fax: +255 024 2230027
Mobile: +255 77 000000
Pemba Office
P.O.Box 112
Chake chake, Pemba
Tel.: +255 024 2452294
Fax: +255 024 2452291

Us

Home About Us Departments

External Links

IPA OCAG ZAECA