Govt. Logo

OFISI YA RAIS - UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

Govt. Logo

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA ZAZNZIBAR

Posted: 2020-03-06 15:16:22
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Afya Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1.Muuguzi Daraja la III “Nafasi 89” Unguja na “Nafasi 40” Pemba

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya “Uuguzi” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Muhudumu wa Afya Daraja la III “Nafasi 60” Unguja

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.

3.Afisa Muuguzi Daraja la II “Nafasi 8” Unguja na“Nafasi 4” Pemba

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza ya “Uuguzi” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4.Mlinzi Daraja la III “Nafasi 20” Unguja

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)

5.Afisa Ushauri Nasaha Daraja la II “Nafasi 9” Unguja na “Nafasi 3” Pemba

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya “Ushauri Nasaha ” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6.Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la III “Nafasi 10” Unguja na “Nafasi 5” Pemba

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya “Environmental Health” kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 13 Machi, 2020 wakati wa saa za kazi.

Contacts

Main Office
P.O.Box 3356
Zanzibar, Tanzania
Tel.: +255 024 2230038
Fax: +255 024 2230027
Mobile: +255 77 000000
Pemba Office
P.O.Box 112
Chake chake, Pemba
Tel.: +255 024 2452294
Fax: +255 024 2452291

Us

Home About Us Departments

External Links

IPA OCAG ZAECA