Govt. Logo

OFISI YA RAIS - KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Govt. Logo

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

Posted: 2022-07-27 16:53:35
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi za ualimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa ajili ya Skuli za Maandalizi, Msingi na Sekondari Unguja na Pemba Kama ifuatavyo:-
1. MWALIMU “GRADE A” SANAA DARAJA LA II -ZPSF-10 Nafasi 29 Unguja na Pemba
Ufafanuzi wa nafasi hizo ni kama ifuatavyo:
MASOMO IDADI
History-English 10
Geography- English 19
JUMLA 29

Sifa za waombaji.
Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 46
Awe mwenye Shahada ya Kwanza ya Ualimu wa Sanaa katika tahsusi (combination) za masomo ya Geography- English au History-English kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kufundisha katika Skuli za Sekondari
ii. Kutathmini maendeleo ya wanafunzi na kutoa taarifa kwa uongozi;
iii. Kutoa taarifa za tathmini hizo kwa uongozi wa skuli;
iv. Kutunga na kusahihisha mitihani ya wanafunzi.
v. Kuandaa kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi.
vi. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na ya mwaka;


2. MWALIMU “GRADE A” SAYANSI DARAJA LA II ZPSG-02. Nafasi 221 Unguja na Pemba
Ufafanuzi wa nafasi hizo ni kama ifuatavyo:
MASOMO IDADI
Biology 20
Chemistry 20
Physics 80
Mathematics 100
Agricultural Science 1

Sifa za waombaji.
Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 46
Awe mwenye Shahada ya Kwanza ya Ualimu wa Sayansi katika katika masomo ya Biology, Chemistry, Physics na Mathematics au Agricultural science kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kufundisha katika Skuli za Sekondari
ii. Kutathmini maendeleo ya wanafunzi na kutoa taarifa kwa uongozi;
iii. Kutoa taarifa za tathmini hizo kwa uongozi wa skuli;
iv. Kutunga na kusahihisha mitihani ya wanafunzi.
v. Kuandaa kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi.
vi. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na ya mwaka;
vii. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.


MWALIMU “GRADE B” DARAJA LA III (ZPSD-06/SANAA) (ZPSD-08/SAYANSI) Nafasi 590 Unguja na Pemba
Ufafanuzi wa nafasi hizo ni kama ifuatavyo:


WILAYA MASOMO YA SANAA MASOMO YA SAYANSI JUMLA
Wilaya ya Wete 30 70 100
Wilaya ya Micheweni 30 70 100
Wilaya ya Mkoani 30 70 100
Wilaya ya Chakechake 50 50 100
Wilaya ya Kaskazini A 50 50 100
Wilaya ya Kati 40 40 80
Wilaya ya Kusini 5 5 10

Sifa za waombaji.
Awe Mzanzibari mwenye umri usizidi miaka 46
Awe na Stashahada ya Ualimu wa Msingi ( Diploma in Primary Education) ya Sanaa/Sayansi, kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kufundisha Skuli za Msingi.
ii. Kutathmini maendeleo ya Wanafunzi.
iii. Kutoa taarifa za tathmini na matokeo mbali mbali kwa uongozi wa Skuli.
iv. Kujenga mashirikiano kati ya walimu, Wanafunzi na Wazazi au Walezi.
v. Kuandaa na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya Wanafunzi.
vi. Kutoa ushauri nasaha kwa Wanafunzi, Wazazi na Walezi.
vii. Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani Skuli katika ngazi anayofundisha.
viii. Kutathmini Mitaala ya masomo wanayofundisha.

3. MWALIMU “GRADE C” DARAJA LA III- ZPSC-06 Nafasi 488 Unguja na Pemba
Ufafanuzi wa nafasi hizo ni kama ifuatavyo:

WILAYA JUMLA
Wilaya ya Wete 70
Wilaya ya Micheweni 88
Wilaya ya Mkoani 50
Wilaya ya Chakechake 50
Wilaya ya Kaskazini A 40
Wilaya ya Kaskazini B 40
Wilaya ya Mjini 20
Wilaya ya Magharib A 30
Wilaya ya Magharib B 40
Wilaya ya Kati 40
Wilaya ya Kusini 20


Sifa za waombaji.
Awe Mzanzibari mwenye umri usiopungua miaka 46
Awe mwenye Cheti cha Ualimu wa Maandalinzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Majukumu
i. Kufundisha Skuli za Maandalizi
ii. Kutathmini maendeleo ya Wanafunzi;
iii. Kutoa taarifa za tathmini hizo kwa uongozi wa Skuli;
iv. Kusahihisha mitihani ya Skuli na kitaifa katika ngazi ya Msingi.
v. Kuandaa na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya Wanafunzi.
vi. Kujenga mazingira yanayofaa kufundishia/kujifunzia.
vii. Kuhimiza na kufuatilia mahudhurio ya Wanafunzi.
viii. Kusimamamia masula ya nidhamu ya Wanafunzi
ix. Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani Skuli katika ngazi anayofundisha.
x. Kuandaa maazimio ya kazi na maandalio ya masomo.
xi. Kuweka kumbukumbu za kila siku za masomo anyofundisha;
xii. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka;

Jinsi ya Kuomba:
• Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektronic wa ajira (Zanajira) kupitia anuani ifuatayo:- https://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 01 Agosti, 2022 hadi tarehe 21 Agosti, 2022

• Mfumo huo pia unapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz

• Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi ya kazi pamoja na Wilaya anayoiombea.


TANBIHI:
Tume ya Utumishi Serikalini inawatahadharisha waombaji wote kwamba ajira zinatolewa bure. Hivyo, wanatakiwa kujiepusha na Matapeli wanaotumia nafasi hizi kwa kujipatia kipato kisicho cha halali.


Contacts

Main Office
P.O.Box 3356
Zanzibar, Tanzania
Tel.: +255 024 2230038
Fax: +255 024 2230027
Webmail: info@utumishismz.go.tz
Website: www.utumishismz.go.tz
Pemba Office
P.O.Box 112
Chake chake, Pemba
Tel.: +255 024 2452294
Fax: +255 024 2452291

Us

Home About Us Departments

External Links

IPA OCAG ZAECA EGOZ MUFTI