NAFASI ZA KAZI OFISI YA MAMLAKA YA KUZUIA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI ZANZIBAR

Posted: 2022-11-22 14:35:42
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi kama ifuatavyo:-

1. Afisa Uchunguzi Muhandisi Mifumo Daraja la II ‘Nafasi 2’-Unguja.
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu shahada ya kwanza katika fani ya Computer Science, Computer Engineerig, Information Systems Engineering na nyengine zinazolingana na hizo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amepata mafunzo ya Ethical Hacker Certification katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar maombi yake yatazingatiwa.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai.

2. Afisa Uchunguzi Muhandisi Majengo (Civil Engineer) Daraja la II ‘Nafasi 2’ - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika moja ya fani zifuatazo Civil Engineering, Constructive Management, Structuring Engineering au fani nyengine zinazolingana na hizo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amethibitishwa na Bodi ya Usanifu Wahandisi na wakadiriaji majengo inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai.

3. Afisa Uchunguzi Mthamini (Valuer) Daraja la II – ‘Nafasi 2’ – Unguja.
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani Valuation au fani inayolingana nayo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amethibtishwa na Bodi ya Wathamini inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai..

4. Afisa Uchunguzi Wakadiriaji Majengo (Quantity Surveyor) Daraja la II ‘Nafasi 2’ - Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu Shahada ya kwanza katika fani ya Quantity Surveying, Building Economics au fani inayolingana nayo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe amethibitishwa na Bodi ya Usanifu Wahandisi na Wakadiriaji majengo inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai.

5. Afisa Uchunguzi Kodi Daraja la II ‘Nafasi 1’ - Unguja
Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe na Shahada ya kwanza ya Tax, Hisabati au fani inayolingana nayo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai.

6. Afisa Uchunguzi Daraja la II (ZPSI-02) ‘Nafasi 2’-Pemba.
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika moja ya fani zifuatazo Statistics, Tax, Civil Engineering, Constructive Management, Quantity Surveying, Computer Science, Computer Engineering au fani nyengine zinazolingana na hizo kutoka katika vyuo vivyotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai. Muombaji aliepata mafunzo ya JKU au JKT maombi yake yatazingatiwa.

7. Afisa IT Daraja la II (ZPSI-02) ‘Nafasi 1’-Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 35.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika moja ya fani zifuatazo, Sayansi ya Computer, Technologia ya Habari na Mawasiliano na nyengine zinazolingana nazo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
• Awe na afya njema na asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la jinai. Muombaji aliepata mafunzo ya JKU au JKT atazingatiwa.

Jinsi ya Kuomba:
• Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa Kielektronic wa maombi ya ajira (Zanajira) kupitia anuani ifuatayo:- http://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 22 Novemba, 2022 hadi tarehe 06 Disemba, 2022.

• Mfumo huo pia unapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz

• Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P. 1587,
ZANZIBAR.

• Muombaji anatakiwa kuanisha nafasi ya kazi aliyoombea

Kwa msaada wa kitalamu wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kupitia email: helpdesk@zanajira.go.tz au Simu Nam. 0773101012.
Close
Close