NAFASI YA KAZI SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR (ZBC)

Posted: 2022-11-25 13:33:48
Tume ya Utumishi Serikalini kwa niaba ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) inatangaza nafasi ya kazi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Utangulizi:

Shirika la Utangazaji wa Zanzibar (ZBC) imeundwa kwa Sheria Namba 4 ya mwaka 2013. Shirika lina bodi ya ushauri na linaongozwa na Mkurugenzi Mkuu. Malengo makuu ya Shirika ni pamoja na kutoa elimu, burudani na taaluma kwa Umma, kuandaa na kurusha matangazo ya Televisheni na Redio ambayo yatachangia katika maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi, Kiutamaduni na Kisiasa ambayo yanalenga katika kujenga umoja na utengamano wa Kiutamaduni na kuliendesha Shirika kibiashara.

Serikali inatafuta Mkurugenzi Mkuu ambae ana sifa na uwezo wa kuliendesha Shirika kwa ufanisi zaidi na kukidhi matarajio ya Serikali na Wananchi kwa jumla.

Sifa za Muombaji:
Awe na angalau Shahada ya pili au inayolingana nayo katika moja au zaidi ya moja ya fani za Mawasiliano ya Umma, Uongozi wa Biashara, Utawala wa Umma na Teknolojia ya Habari kutoka kwenye Chuo Kikuu au Taasisi inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Awe na angalau uzoefu unaohitajika usiopunguwa miaka mitano (5) katika tasnia ya Utangazaji.
Awe na Utaalamu, Ujuzi, na Uzoefu wa kutosha katika tasnia ya utangazaji.

Sifa za Ziada
Awe na Utaalamu wa Teknolojia mpya ya Habari (New Media Management)
Awe na Utaalamu na uzoefu wa Uongozi wa Habari (Media Management)
Awe na Uwezo wa kuunganisha watu (Team Builder)
Kutoa maamuzi na kusimamia utekelezaji (Decision Maker and Follow up)
Awe Mbunifu (Innovator)
Awe na uwezo mkubwa wa kutafakari kwa kina (Critical Thinker)

MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia shughuli zote za Shirika za kila siku
Kuandaa na Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Shirika wa miaka mitano
Kuhakikisha mali za Shirika zinatumika kwa usahihi na uangalifu
Kusimamia matangazo ya ZBC TV, REDIO, ZBC2 na kuhakikisha vipindi vinazalishwa kwa mujibu wa Sera na Sheria.

Jinsi ya Kuomba:
Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P. 1587,
ZANZIBAR.

Hati zote zitakazoungwanishwa na Maombi ya ajira zitumwe katika muundo wa PDF kwenye email ifuatayo maombizbc@zanajira.go.tz kuanzia tarehe 25 Novemba, 2022 hadi tarehe 20 Disemba, 2022.
Close
Close