Uzinduzi wa Kituo cha hospitali ya wazamiaji KMKM (Decompression Chamber)

news phpto

Picha kwa hisani ya kitengo cha habari

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi na utawala Bora Mh Haroun Ali Suleiman amesema mpango wa kujenga hospitali ambayo ndani yake kuna kifaa cha kuokoa maisha watu wanaopata majanga ya kuzama baharini decompression chamber ), kutasaidia kupunga idadi ya vifo na majeruhi wanaopata majanga hayo.

Akiweka mawe ya msingi katika jengo la hospitali ya uwokozi wa wazamiaji na wananchi ( Decompression Chamber ) huko nungwi mnarani amesema hatua hiyo itasaidia kupatikana huduma za mwanzo wa urahisi.

Amesema ivi sasa kumekua na majanga mengi ya watu kuzaa baharini hasa wale wanaokaa karibu na maeneo ya bahari hivyo kuwepo kwa kituo hicho katika eneo la nungwi kutasaidia kupunga maafa kwa wenyeji na wegeni wanaotoka nje ya Zanzibar .

Aidha amekiomba kikosi cha kmkm kukilinda kituo hicho sambamba na kutumia kifaa hicho wakati wa huduma za dharura na sio kutumia katika shughulu nyengine.

Naibu mkuu wa kmkm kepteni khatib khamis mwadini amesema kuwepo kwa hospitali ambayo ndani yake kuna mtambo wa kusaidia waathirika kuwapatia huduma ya kwanza baada ya uokozi ambapo awali walikua hawaipati na wengini wao kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

Akisoma taarifa ya kitaalamu Naibu katibu mkuu kutoka afisi ya Rais tamisemi Mikidadi Mbarouk Mzee amesema ujenzi huo umegharimu zaidi bilioni mbili zilizopangwa kutumika na utaleta tija kwa wananchi kwani utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Zanzibar na nje ya Zanzibar .

Mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja Mh Ayoub Muhammed Mahmoud amesema maamuzi ya serikali ya awamu ya nane kujenga hospitali katika jimbo la nungwi ni maamuzi sahihi kwani kumekua Na majanga mengi ya watu kuzama na wengine kupoteza maisha hivyo kuwepo kwa kituo hicho kutasaidia kupunguza majanga hayo.

Close
Close