Taarifa ya Utekelezaji wa majumusho ya Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora

news phpto

Kutoka kitengo cha Habari

Ofisi Raisi Katiba sheria Utumishi na Utawala bora imesema imelenga kutekeleza mipango mbali mbali ikiwemo mpango wa rasilimali watu na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kieletroniki Ili kuimarisha utoaji wa huduma Bora kwa wananchi.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo kwa kipindi chà oktoba Hadi Disemba 2022 Katibu Mkuu Mansura Mosi kassim amesema mpango huo unatekelezwa katika kipindi chà mwaka wa fedha 2022/2023 Ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu na kuleta tija kwa Taifa.

Amesema Ofisi hiyo inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sera sheria na miongozo mbali mbali ya serikali Ili kuimarisha maslahi ya watumishi na kudhibiti vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar.

Aidha amesefahamisha kuwa katika kipindi chà Oktoba Hadi Disemba 2022 Ofisi imekusanya bilioni Moja,milioni miamoja thelathini na nne,laki saba,elfu nne na mia mbili na Moja(1,134,704,201),sawa na asilimia 91% kwa upande wa Zanzibar na upande pemba milioni mia moja na arubaini nane ,laki tano themanini na tano elfu mia moja na arubaini na nne (148,585,144) sawa na asilimia 99% ya makadirio ya mapato walio kusudia kukusanya katika kipindi hicho.

Kamati ya kusimamia Ofisi ya Viongozi wakuu wa kitaifa ya baraza la wawakilishi chini ya mwenyekiti wake Mhe Machano Othman Saidi ameiyomba Ofisi kutafuta eneo ambalo kitajengwa chuo chà IPA kwa upande wa pemba Ili kuepusha Serikali kupata hasara kutokana na eneo hilo kutokidhi haja.

Nae kaimu waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Katiba Sheria Utumishi Utawala Bora Mhe Hamza Hassan Juma amewataka watendaji kuhakikisha wanafanya kazi kwa udalifu na kutatua matatizo ya watumishi kwa wakati Ili kuepusha migogoro kati yao na wafanyakazi.

Close
Close