Waziri wanchi(0R)Utumishi wa Umma na Utawala Bora akizungumzia masuala ya Rushwa

Waziri wanchi(0R)utumishi wa umma na utawala bora Haroun Ali Suleiman amesema rushwa ni maradhi yanayoikabili jamii,na yanahitaji kufanyiwa ufumbuzi wa kina kabla athari haijajitokeza kwa haraka zaidi.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja na ujumbe aliokutana nao kutoka umoja wa afrika wa kuzuia na kupamba na rushwa kilichofanyika katika ukumbi wa utumishi wa umma na utawala bora mazizini.

Amesema endapo elimu ya rushwa itaendelea kutolewa mijini na vijijini tatizo lilokuwepo linaweza kupatiwa ufumbuzi na kupelekea kupatikana kwa maendeleo zaidi .

Aidha amesema ujumbe huo umefika Zanzibar kwa lengo la kufanya tathmin ya utekelezaji mkataba wa umoja wa afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa.

Nae mwenyekiti wa ujumbe kutoka umoja wa afrika wa kuzuia na kupambana na rushwa nd.MIAROM BEGATO Ameishukuru serikali ya watu wa Zanzibar kwa hatua iliyofikia katika masuala yakuzuia na kupambana na rushwa Zanzibar.

Close
Close