Kaskazini Unguja na Uchumi wa Buluu

news phpto

Picha kwa hisani ya kitengo cha habari

Wavuvi wa mkoa wa kaskazini Unguja wameiyomba Serikali kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusiana na dhana ya Uchumi wa Buluu ili wavuvi hao wanufaike na fursa mbali mbali zinazopatikana kupitia sekta hiyo.

Wakitoa maoni yao mara baada ya kukutana maafisa kutoka Idara ya Msaada wa Kisheria huko Mkokotoni wavuvi hao wamesema licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha dhana ya uchumi wa buluu lakini bado hawajanufaika ipasavyo kupitia sekta hiyo kwa kukosa taaluma sahihi juu ya namna ya kupata vifaa vya uvuvi na ukosefu wa taaluma ya ufugaji wa mazao ya bahari.

Aidha wameleza kuwa licha ya utayari wa baadhi yao kujisajili kupitia Idara husika lakini bado wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbali mbali wakati wa utekelezaji wa shughuli zao za uvuvi ikiwemo kutotambulika leseni zao za uvuvi pale wanapotoka maeneo ya nje ya visiwa vya Zanzibar

Afisa uvuvi Wilaya ya kaskazini "A" Idi Mohammed Ali na fisa Sheria Baraza la mji kaskazini "A "Bimkubwa Ghazal Amar

Wamewasisitiza wavuvi hao kufuata utaratibu uliowekwa ikiwemo kuvisajili vikundi vyao na kukata lessen ili waweze kutambulika kisheria jambo ambalo litawawezesha wavuvi hao kunufaika na fursa mbali mbali zitakazotolewa na Serikali kupitia sekta ya uvuvi.

Ali haji Hassan ni Afisa Sheria kutoka Idara ya Msaada wa Kisheria kutoka Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora amewataka wavuvi hao kuwatumia Maafisa Msaada wa Kisheria pindi wanapokabiliwa na matatizo mbali mbali ya kisheria ili kuweza kupata msaada wa kisheria

Close
Close