KUENDELEA KUSHIKAMANA NA KULETA UMOJA KATIKA JAMII

news phpto

Mhe.Haroun Ali Suleiman

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA HAROUN ALI SULEIMAN AMEWATAKA VIONGOZI WA JUMUIYA YA FISABILILLAH KUENDELEA KUSHIKAMANA NA KULETA UMOJA KATIKA JAMII, JAMBO AMBALO NDIO NGUZO INAYOILETEA AMANI NA UTULIVU KATIKA NCHI.

KAULI HIYO AMEITOA HUKO OFISINI KWAKE MAZIZINI WAKATI ALIPOKUTANA NA UJUMBE HUO KUTOKA JUMUIYA YA FISABILILLAH MARKAZ ZANZIBAR.

AMESEMA ENDAPO VIONGOZI WATASIMAMIA NA KUENDELEZA MASHIRIKIANO YENYE NGUVU NA UMOJA YATAWEZA KUIWEKA NCHI KATIKA AMANI

AMEWAOMBA VIONGOZI HAO KUMSAIDIA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,KWA KUIOMBEA NCHI YETU KUWA NA AMANI NA KUWEZA KUPATA VIONGOZI WAADILIFU.

MAPEMA MWENYEKITI WA FISABILILLAH AMIRI ALI KHAMIS MWINYI AMESEMA JITIMIAI HIYO HUU NI MWAKA 11 HIVYO WANASHUKURU SERIKALI KWA NA WATENDAJI WOTE KWA KUHAKIKISHA WANALIFANIKISHA SUALA HILI.

NAE MAKAMO MWENYEKITI WA JUJMUIYA HIYO AMIR WAKATI HASSAN BAKAR AMESEMA LENGO HASA NI KUWASHUKURU WATENDAJI WOTE KWA KUSHIRIKI BILA YA KUJALI VYAMA VYA SIASA WALA MADHEHEBU NA KUWAKUMBUSHA MASHEHE MBALIMBA UKUMBUSHO WENYE KUFAA.

AIDHA WANAHAMASISHA JAMII KUPUNGUZA MAMBO YA UDHALILISHAJI JAMBO AMBALO NDIO CHANGAMOTO KUBWA INAYO IKABILI JAMII KWA SASA.

Close
Close