Govt. Logo

OFISI YA RAIS - KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Govt. Logo

EID AL ADHA.
AFISI YA RAIS KATIBA,SHERIA NA UTAWALA BORA inawatakia waislamu wote iddi njema

Mahkama kuu vuga
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman amewataka majaji na mahakimu kuwa makini na waadilifu katika utendaji wao wa kazi zao za kila siku ili kuondoa changamoto za hapa na pale.

Mahkama kuu vuga
Waziri Haroun Ali Suleiman amesisitiza kuendelea kupiga vita suala la udhalilishaji na madawa ya kulevya kwa kuchukuliwa hatua madhubuti za kisheria.

Mahkama kuu vuga
Jaji Mkuu wa mahakama kuu ya vuga Omar Otman Makungu amesema kutokana na uhaba wa nafasi katika jengo hilo inapelekea uzorotaji wa kuendesha kesi mahakamani

Mahkama kuu Vuga
Mrajis wa mahakama kuu Mohamed Ali Mohamed amesema juhudi mbali mbalizinachukuliwa kuhakikisha masuala ya udhalilishaji yanapungua na tatizo uchukuaji ushahidi na utoaji maelezo unafanyiwa kazi ili kuhakikisha kesizinatolewa ufumbuzi kwa haraka.

Mahkama kuu Vuga
Baadhi ya washiriki walioshiriki katika ziara hiyo ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katika Sheria Utumishi na Utawala Bora ya kuonana na majaji na kuzungumza naom iliyofanyika mahakama kuu Vuga

Mahkama kuu Vuga
Baadhi ya washiriki walioshiriki katika ziara hiyo ya Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katika Sheria Utumishi na Utawala Bora ya kuonana na majaji na kuzungumza naom iliyofanyika mahakama kuu Vuga

Mahkama kuu Vuga
Kaimu Mkurugenzi Mashtaka Muumin Khamis Kombo akizungumza machache katika ziara hiyo.

Sherehe ya wiki ya Utumishi
Waziri wa Nchi Katiba ,Sheria Utumishi na Utawala Bara Zanzibar Haroun Ali Suleiman kutoa maelezo machache juu siku ya kilele cha Utumishi wa Umma na kumkaribisha Mgeni Rasmi ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Sherehe ya wiki ya Utumishi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi. Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa watumishi wa Umma wanamchango mkubwa na umuhimu katika Taifa lolote lakini pia wanayo majukumu makubwa ya utoaji wa huduma bora kwa jamii

Sherehe ya wiki ya Utumishi
Dk. Mwinyi amesema ubunifu katika Utumishi wa Umma ni muhimu kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma bora kila inapoezekana tupanue wigo ili kuimarisha utoaji wa huduma zetu na kuwaondolea usumbufu wananchi.

Sherehe ya wiki ya Utumishi
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said akitoa neno la shukran katika siku ya kilele cha Utumishi wa Umma


Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora. Haroun Ali Suleiman akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi siku ya madhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.

Sherehe ya wiki ya Utumishi
Mgeni Rasmi wa madhimisho hayo ambae ni Raisi wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa mwenyeji wake Mwalim Haroun Ali Suleiman.

Sherehe ya wiki ya Utumishi
Dua ya mwisho wa sherehe ya wiki ya siku ya Utumishi iliyosomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar .Ndg Mahmoud Mussa Wadi

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Waziri wa Nchi Afisi ya Raisi, Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora. Haroun Ali Suleiman akiongozana na Makamu wa Kwanza wa Raisi Mh. Othman Masoud Othman kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano Marughubi kwa ajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Katibu Mkuu Afisi ya Raisi Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora. Ndg Seif Shaaban Mwinyi ameishukuru Serikali ya Ujerumani kwa kuiunganisha Taasisi ya HFS na IPA hadi leo hii kufikia hatua nzuri.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Madam Regine Hess amesema wapo tayari kutoa mashirikiano ambayo yana faida katika Taasisi hizo.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Waziri wa Nchi Afisi ya Raisi Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora, Mh. Haroun Ali Suleiman amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo zaid Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi

Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Makamu wa Kwanza wa Raisi Mh. Othman Masoud Othman ambae ndio Mgeni Rasmi wa mafunzo hayo amesema anaamini kuwa mafunzo hayo yataweza kuwajengea uwezo wajumbe hao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binaadamu.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Saba imefanya bidii kubwa kuhakikisha misingi ya utawala bora inafuatwa ili kukuza uchumi na kujenga jamii yenye imani, upendo na mshikamano baina yao, serikali na nchi yao kwa jumla.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika hotu. . . More...>>

Kanuni Bora Za Utumishi Wa Umma Lazima Zitokanane Na Sheria Iliyo Bora

Waziri Wa Nchi (OR) Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman Amesema Kanuni Bora Za Utumishi Wa Umma Lazima Zitokanane Na Sheria Iliyo Bora Inayowashirikisha Wahusika Wake.

Ameyasema Hayo Wakati Wa Ufunguzi Wa Mkutano Wa Mapitio Ya Rasimu Ya Sheria Ya Utumishi Wa Umma Uliowashirikisha Wakurugenzi Wa Uendeshaji Na Utumish. . . More...>>

Waziri wanchi(0R)Utumishi wa Umma na Utawala Bora akizungumzia masuala ya Rushwa

News Photo Waziri wanchi(0R)utumishi wa umma na utawala bora Haroun Ali Suleiman amesema rushwa ni maradhi yanayoikabili jamii,na yanahitaji kufanyiwa ufumbuzi wa kina kabla athari haijajitokeza kwa haraka zaidi.
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja na ujumbe aliokutana nao kutoka umoja wa afrika wa kuzuia na kupamba na rushwa kilichofanyika ka. . . More...>>

Tathmini ya upimaji na utendaji kazi kwa watumishi wa umma

News Photo Watendaji na Viongozi wa( OR )Utumishi wa Umma na Utawala bora wametakiwa kuhakikisha masuala ya upimaji na utendaji kazi kwa watumishi wa umma yanafanywa kwa umakini na uadilifu.
Aliyasema hayo Katibu Mkuu (OR) Utumishi wa Umma na Utawala bora Yakout Hassan Yakout wakati akifungua mafunzo hayo ya tathmini ya upimaji na utendaji kaz. . . More...>>


Contacts

Main Office
P.O.Box 3356
Zanzibar, Tanzania
Tel.: +255 024 2230038
Fax: +255 024 2230027
Webmail: info@utumishismz.go.tz
Website: www.utumishismz.go.tz
Pemba Office
P.O.Box 112
Chake chake, Pemba
Tel.: +255 024 2452294
Fax: +255 024 2452291

Us

Home About Us Departments

External Links

IPA OCAG ZAECA EGOZ MUFTI