Kanuni Bora Za Utumishi Wa Umma Lazima Zitokanane Na Sheria Iliyo Bora

Waziri Wa Nchi (OR) Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman Amesema Kanuni Bora Za Utumishi Wa Umma Lazima Zitokanane Na Sheria Iliyo Bora Inayowashirikisha Wahusika Wake.

Ameyasema Hayo Wakati Wa Ufunguzi Wa Mkutano Wa Mapitio Ya Rasimu Ya Sheria Ya Utumishi Wa Umma Uliowashirikisha Wakurugenzi Wa Uendeshaji Na Utumishi Na Makatibu Wa Tume Za Utumishi Serikalini, Uliofanyikakatika Ukumbi Wa Ofisi Hiyo Uliopo Mazizini Wilaya Ya Magharibi B.

Mhe. Haroun Amewataka Washiriki Wa Mkutano Huo Kutumia Vyema Fursa Muhimu Ya Kupitia Rasimu Ili Kuondoa Changamoto Wanazokumbana Nazo Na Kuweka Sheria Iliyoandaliwa Vizuri.

Mapema Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais Utumishi Wa Umma Na Utawala Bora Ndugu Seif Shaaban Mwinyi Amesisitia Suala La Ufatiliaji Na Mrejesho Katika Kukuza Sekta Ya Utumishi Wa Umma .

Wakati huohuo Maafisa Utumishi Na Wanasheria Wametakiwa Kuweka Umakini Katika Kupitia Marekebisho Ya Sheria Ya Utumishi Ili Kuhakikisha Mapungufu Yaliyokuwepo Yanafanyiwa Kazi.

Close
Close