info@utumishismz.go.tz +255 777 123456

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Majukumu ya Wiza


MAJUKUMU YA OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA

MAJUKUMU KWA UJUMLA
  1. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Mipango na Sera zinazohusiana na sekta husika.
  2. Kufanya na kuendeleza tafiti zinazohusiana na maendeleo ya sekta husika.
  3. Kusimamia Uongozi/Menejimenti ya rasilimali watu, fedha na rasilimali nyenginezo.
  4. Kusimamia shughuli za Ofisi ya Usalama wa Serikali.
  5. Kushughulikia masuala ya kikatiba.
  6. Kusimamia na kuratibu shughuli za Mahkama.
  7. Kusimamia na kuratibu shughuli za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  8. Kusimamia na kuratibu shughuli za Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.
  9. Kusimamia na kuratibu shughuli za Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
  10. Kusimamia na kuratibu shughuli za Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi.
  11. Kusimamia na kuendeleza masuala ya Utawala Bora.
  12. Kusimamia na kutathmini utekelezaji wa sera na maamuzi ya Serikali.
  13. Kusimamia na kuratibu shughuli za Tume ya Kurekebisha Sheria.
  14. Kusimamia masuala ya msaada kisheria na kikatiba.
  15. Kusimamia na kuratibu shughuli za Ofisi ya Mufti.
  16. Kusimamia na kuratibu shughuli za Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.
  17. Kusimamia menejimenti ya utumishi wa umma.
  18. Kusimamia na kuratibu masuala ya uajira, uchaguzi, mafunzo, maendeleo na masuala ya malipo ya watumishi wa umma.
  19. Kusimamia na kuratibu shughuli za Wakala wa Serikali Mtandao.
  20. Kusimamia na kuratibu shughuli Baraza la Mawaziri.
  21. Kusimamia, kuongoza na kuratibu masuala ya msaada wa kisheria.
  22. Kusimamia uongozi, uhifadhi na matumizi ya nyaraka na kumbukumbu za Taifa.
  23. Kusimamia na kuratibu shughuli za Tume ya Maadili ya Viongozi.
  24. Kusimamia shughuli za Chuo cha Utawala wa Umma.
  25. Kusimamia shughuli za Tume ya Utumishi Serikalini.
  26. Kusimamia shughuli za Kamisheni ya Utumishi wa Umma.
  27. Kusimamia shughuli za Tume ya Utumishi wa Mahkama.
  28. Kupokea malalamiko yanayohusu Sekta husika na kuyatafutia ufumbuzi ipasavyo.
  29. MAJUKUMU YA IDARA NA VITENGO VYA OFISI.

    Idara ya Uendeshaji na Utumishi

    Majukumu ya Idara
    1. Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali watu na Utawala kwa Ofisi;
    2. Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Ofisi;
    3. Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji;
    4. Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Ofisi na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa matakwa ya sheria au maagizo maalum;
    5. Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (UKIMWI, jinsia, Mabadiliko ya tabianchi na mambo ya idadi ya watu);
    6. Kuhifadhi na kutunza kumbukumbu zote za Ofisi;
    7. Kusimamia rasilimali zote za Ofisi;
    8. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa mteja.
    9. Kushughulikia na kukadiria upatikanaji wa mahitaji, vifaa na vitendea kazi na kuhakikisha vinatunzwa na kutumika ipasavyo;
    10. Kuandaa, kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa utoaji wa huduma kwa umma;
    11. Kuandaa na kutunza kumbukumbu za watumishi;
    12. Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipango ya mafunzo;
    13. Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi;
    14. Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya kazi; na
    15. Kuratibu utekelezaji wa upimaji utendaji kazi.

    Divisheni ya Uendeshaji

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi;
    2. Kusaidia kusimamia nidhamu ya wafanyakazi;
    3. Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya Ofisi ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano;
    4. Kusimamia majengo na mali za Ofisi;
    5. Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Ofisi;
    6. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na kazi zake kama atavyopangiwa na Mkuu wake.

    Divisheni ya Utumishi

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kutunza Kumbukumbu sahihi za Watumishi wote kulingana na mahali alipo;
    2. Kukusanya Takwimu na kutunza Kumbukumbu zote zinazohusu Mipango ya Watumishi na watumishi wenyewe;
    3. Kukadiria idadi ya Watumishi wanaohitaji Mafunzo;
    4. Kuratibu na Kushughulikia ajira, uthibitishwaji kazini na upandishwaji Vyeo Maofisa wa ngazi mbali mbali;
    5. Kufuatilia na kudhibiti Kumbukumbu za Maafisa wanaokaribia kustaafu Pamoja na kutafiti uwezekano wa upatikanaji wa nafasi za Mafunzo vyuoni;
    6. Kuandaa makisio ya Mishahara ya Watumishi kwa kila mwaka;
    7. Kupanga na kuendesha utafiti kuhusu mahitaji ya Watumishi na upatikanaji wa Watumishi ili kuweza kuainisha uwezo na mahitaji ya Ofisi;
    8. Kufuatilia masuala ya uthibitishaji kwa watumishi, upandishaji vyeo, uhamisho, ubadilishaji kada, kustaafisha, likizo na mengineyo.
    9. Kuandaa ikama (norminal roll) itakayojumuisha makadirio ya mishahara ikiwemo mahitaji halisi ya watumishi pamoja na maslahi ya watumishi wa Baraza.
    10. Kushughulikia maslahi mbali mbali ya watumishi katika wa taasisi.
    11. Kuandaa na kutekeleza mpango wa urithishaji madaraka (succession plans).
    12. Kushughulikia masuala yote ya kiutumishi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo, upimaji utendaji kazi.
    13. Kushughulikia malalamiko, migogoro na matatizo ya wafanyakazi.
    14. Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa Miundo ya Utumishi na taasisi.

    Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kutafuta Kumbukumbu/Nyaraka/Mafaili yanayohitajiwa na watumishi wa Ofisi
    2. Kupokea na kudhibiti na kutunza kumbukumbu za Ofisi
    3. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga Kumbukumbu/Nyaraka katika makundi kulingana na mada husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi;
    4. Kuweka/kupanga Kumbukumbu/Nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika Masjala na vyumba vya kuhifadhi kumbukumbu tuli za Ofisi
    5. Kuweka na kutunza kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika Mafaili;
    6. Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka kwa maafisa mbali mbali na Taasisi za Serikali;
    7. Kuhifadhi Majalada yaliyofungwa kwa Kumbukumbu za baadae;
    8. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na kazi zake kama atavyopangiwa na Mkuu wake.

    Idara ya Mipango Sera na Utafiti

    Majukumu ya Idara
    1. Kuandaa Mpango wa Mwaka na Mpango Mkakati wa maendeleo wa muda wa Kati wa Ofisi;
    2. Kufuatilia, kukusanya na kuratibu Mipango ya Maendeleo ya Taasisi;
    3. Kuhakikisha kuwa rasilimali na fedha za Misaada inatumika vizuri;
    4. Kutoa utaalamu na huduma kwa ajili ya Maandalizi, Mapitio, Ufuatiliaji na Sera mbalimbali za Sekta;
    5. Kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji (disseminate) wa Takwimu mbalimbali za Ofisi kwa kushirikiana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali;
    6. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango kazi na mpango mkakati wa Ofisi;
    7. Kufanya ufatiliaji na tathmini wa utekelezaji mpango kazi wa Ofisi;
    8. Kusimamia, kufanya mapitio na tathmini ya Sera, Mipango, Programu na Miradi mbali mbali ya Ofisi;
    9. Kuratibu shughuli za tafiti na kutayarisha maelezo ya kisera kutokana na tafiti hizo;
    10. Kuandaa bajeti ya Ofisi.

    Divisheni ya Ufuatiliaji Utafiti na Tathmini

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kuandaa Viashiria vya taarifa ya ufuatiliaji kwa kuzingatia mahitaji ya Mpango Kazi wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora;
    2. Kuandaa na kushiriki ziara mbali mbali za Ufuatiliaji, Ukaguzi wa miradi ya maendeleo na Tathmini zinazofanyika kwa kuhakikisha zinafuata Mifumo iliyokubalika katika ukusanyaji wa taarifa ili ziweze kusaidia katika kutoa maamuzi ya Uongozi;
    3. Kuanzisha Mfumo bora wa kukusanya matokeo ya Tathmini na Ufuatiliaji;
    4. Kufuatilia utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Ofisi;
    5. Kutayarisha Ripoti za utekelezaji wa majukumu ya Ofisi za robo mwaka, nusu, na mwaka
    6. Kukusanya taarifa za uchambuzi wa Takwimu/Taarifa zinazohitajika katika kutayarisha Sera, Mipango pamoja na mapendekezo ya bajeti;
    7. Kushiriki katika kutayarisha Mipango, Programu na shughuli za bajeti za Ofisi ikiwemo kutayarisha Malengo halisi ya utekelezaji na Viashiria;
    8. Kutoa ushauri wa kitaalamu ikiwemo kuanzisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ndani ya Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora;

    Divisheni ya Maendeleo ya Sera

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kutayarisha karatasi ya dhamira (concept paper) ya Sera zinazohitajika na kushauri kwa Uongozi wa Ofisi;
    2. Kuchambua Sera zilizopo za Ofisi Kiuchumi, Kijamii na Kiutawala kwa ajili ya kuweka mazingira bora ya utekelezaji;
    3. Kuwasiliana na kufanya kazi pamoja na Tume ya Mipango wakati wa kutayarisha na kutekeleza Sera mpya ili kuhakikisha kuwa zinakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango ya Kitaifa ikiwemo Mpango wa Maendeleo ya Zanzibar, Dira ya Maendeleo ya 2050 pamoja na Mipango Mikakati ya Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

    Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kukusanya taarifa na kutayarisha Mpango Kazi wa Mwaka pamoja na Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Ofisi kwa kushirikiana na Tume ya Mipango ili kuhakikisha mipango hiyo inakwenda sambamba na utekelezaji wa Mipango wa Maendeleo.
    2. Kuratibu utayarishaji wa mpango mkakati na utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi;
    3. Kukusanya Taarifa za Miradi, Programu na Mipango kazi ya Ofisi;
    4. Kujenga uelewa na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Ofisi na kutayarisha Bajeti ya Ofisi;
    5. Kukusanya taarifa za mapitio ya utekelezaji za kipindi cha muda wa Kati na Mwaka za Ofisi;
    6. Kuratibu utekelezaji wa maamuzi ya Serikali juu ya masuala ya Mipango na Uongozi wa masuala ya kiuchumi ya Ofisi;
    7. Kukusanya Taarifa na Takwimu zinazohitajika katika kubainisha vipaumbele vya ustawi na maendeleo ya jamii;
    8. Kuchambua na kutafsiri (interpret)Takwimu na Taarifa mbalimbali za kiuchumi;
    9. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa majukumu ya kazi husika.

    Idara ya Miundo na Maslahi ya Watumishi.

    Majukumu ya Idara
    1. Kuratibu uanzishwaji na kusimamia utekelezaji wa Mikataba wa Utoaji wa Huduma katika Ofisi, Idara na Taasisi za Serikali;
    2. Kutayarisha na kufanya mapitio ya Muongozo na Fomu ya Upimaji Utendaji Kazi, pamoja na kufanya Tathmini ya utekelezaji wa Upimaji Utendaji Kazi katika Taasisi za Serikali;
    3. Kutayarisha Miundo ya Utumishi na Miundo ya Taasisi pamoja na kuifanyia mapitio na kutoa Miongozo/utaalamu kabla ya Miundo hiyo kuwasilishwa Kamisheni ya utumishi wa Umma.
    4. Kutayarisha, kuandaa, kutoa Nyaraka, Miongozo na Matoleo mbalimbali yanayohusu masuala ya Kiutumishi katika Ofisi na Taasisi za Serikali Pamoja na kujenga uelewa wa miongozo hiyo;
    5. Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Utumishi wa Umma kwa kutoa mafunzo, ikiwemo malipo na kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwa Wananchi;
    6. Kusimamia, kuandaa na kufanya marekebisho, kuweka au kuondoa kizuizi cha Mishahara ya Watumishi wa Umma kwa Mtumishi pamoja na kuimarisha mfumo wa malipo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya Utumishi wa Umma za Mwaka 2014.
    7. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa majukumu ya kazi husika.

    Divisheni ya Uchambuzi Kazi Miundo na Mifumo

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kushauri juu ya uanzishwaji wa mifumo inayohusiana na usimamizi wa utumishi wa umma.
    2. Kuratibu uanzishwaji, na kusimamia utekelezaji wa Mikataba wa Utoaji wa Huduma katika Ofisi, Idara na Taasisi za Serikali;
    3. Kutayarisha na kufanya mapitio ya Muongozo na Fomu ya Upimaji Utendaji Kazi, pamoja na kufanya Tathmini ya utekelezaji Upimaji Utendaji Kazi katika Taasisi za Serikali;
    4. Kutayarisha Miundo ya Utumishi na Miundo ya Taasisi pamoja na kuifanyia mapitio na kutoa Miongozo/utaalamu kabla ya Miundo hiyo kuwasilishwa Kamisheni ya utumishi wa Umma.
    5. Kufanya uchambuzi wa miundo mbali mbali itakayowasilishwa Wizarani.
    6. Kutayarisha miundo iliyoidhinishwa/kuridhiwa kufuatia maoni na mapendekezo.
    7. Kusimamia uanzishwaji, na utekelezaji wa Mkataba wa Utoaji wa Huduma kwa Taasisi Umma;
    8. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa majukumu ya kazi husika.

    Divisheni ya Maslahi ya Watumishi

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kushauri juu ya uanzishwaji wa stahiki zinazohusiana na Maslahi ya utumishi wa umma.
    2. Kufanya Marekebisho ya Mishahara na Maposho na Stahiki nyenginezo katika Utumishi wa Umma.
    3. Kuweka/na kuondoa kizuizi katika Mshahara kwa Mtumishi kutokana na sababu mbalimbali kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya Utumishi wa Umma za Mwaka 2014.
    4. Kusimamia Uanzishaji wa Maslahi yakijumuisha Posho na Stahiki mbali mbali kwa Watumishi wa Umma.
    5. Kuhakikisha Malipo ya Stahiki zinatekelezwa kwa Mujibu wa Muongozo wa Mfumo wa Malipo Zanzibar.
    6. Kusimamia, kuandaa na kufanya marekebisho ya Mishahara ikijumuisha Mtumishi anaporudi masomoni, kufariki, au likizo bila ya malipo n.k);
    7. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa majukumu ya kazi husika.

    Divisheni ya Matoleo na Miongozo.

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kutayarisha Nyaraka mbalimbali zinazohusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Sehemu nyengine za Idara na kuziwasilisha Serikalini kwa mujibu wa taratibu zilizopo;
    2. Kuandaa, kutoa Miongozo na Matoleo mbalimbali yanayohusu masuala ya Kiutumishi katika Ofisi na Taasisi za Serikali;
    3. Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Utumishi wa Umma, ikiwemo malipo na kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwa Wananchi;
    4. Kuratibu na kuandaa rasimu ya Marekebisho ya Sera, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Wahusika mbalimbali wa Maendeleo;
    5. Kutoa Elimu/Mafunzo na ufafanuzi wa masuala yanayohusu Sera, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Ofisi, Idara na Taasisi za Serikali.
    6. Kuzitangaza kanuni kama zitavyotolewa na Sheria ya Utumishi wa Umma au Sheria nyengine.
    7. Kupitia taratibu katika taasisi za usimamizi wa Utumishi wa Umma na kutoa maelekezo ya kufuata Sheria za Utumishi wa Umma, kanuni, viwango vya utumishi na mwenendo mzuri wa Utumishi wa Umma katika sehemu yoyote.

    Divisheni ya Ushughulikiaji wa Malalamiko na Ushauri

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kupokea na kufuatilia malalamiko mbalimbali yanayowasiliswa;
    2. Kupitia malalamiko yaliyopokelewa na kutoa ushauri wa kitaalamu pale inapohitajika;
    3. Kutayarisha maoni na mapendekezo kwa mujibu sheria na kanuni za kiutumishi kutokana na malalamiko yanayowasilishwa.
    4. Kufanya tathmini na Ufuatiliaji wa malalamiko yanayowasilishwa.
    5. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa kazi za Divisheni.

    Idara ya Mipango ya Rasilimali Watu

    Majukumu ya Idara
    1. Kuandaa Sera na Miongozo inayohusu Mipango ya Rasilimali Watu na kuratibu utekelezaji wake na kusimamia matumizi bora ya Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma (Optimum Utilization of HR)
    2. Kuratibu na kusimamia utekezaji wa Mpango wa miaka mitano (5) wa Rasilimali Watu na Mpango wa Uandaaji Viongozi (Succession Plan) katika Taasisi za Umma;
    3. Kuratibu Mikutano ya Kila Robo Mwaka ya Wakurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji;
    4. Kutoa vibali vya Ajira, uhamisho na kutoa msaada wa kitaalamu kwa Taasisi za Umma kuhusiana na Mipango ya Rasilimali Watu;
    5. Kuandaa Sera na Miongozo inayohusu mafunzo katika Utumishi wa Umma Pamoja na kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Mafunzo katika Taasisi za Umma.
    6. Kutafuta na kuratibu upatikanaji wa fursa za Mafunzo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na Taasisi za Kitaaluma na kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mikataba ya Mafunzo kwa Watumishi wa Umma wanapokwenda masomoni
    7. Kutoa Ushauri wa kitaalamu kwa Taasisi za Umma kuhusu utekelezaji wa Sera na Miongozo inayosimamia Mafunzo ya watumishi wa Umma.
    8. Kutoa msaada wa kitaalamu kwa Watumiaji wa Mfumo wa uwekaji wa taarifa za watumishi wa umma katika Taasisi za umma na kutunza taarifa za Watumishi wa Umma katika Mfumo wa Kielektroniki (Human Resource Management Information Systerm - Database); na
    9. Kutunza taarifa za Taluma za watumishi wa umma.

    Divisheni ya Mipango ya Rasilimali Watu

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kuandaa Sera na Miongozo inayohusu Mipango ya Rasilimali Watu na kuratibu utekelezaji wake;
    2. Kuratibu na kusimamia utekezaji wa Mpango wa miaka mitano (5) wa Rasilimali Watu;
    3. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Uandaaji Viongozi (Succession Plan) katika Taasisi za Umma;
    4. Kusimamia matumizi bora ya Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma (Optimum Utilization of HR);
    5. Kuratibu Mikutano ya Kila Robo Mwaka ya Wakurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji;
    6. Kutoa Vibali vya Ajira kwa Taasisi za Umma;
    7. Kufanya uhamisho wa Watumishi wa Umma;
    8. Kutoa msaada wa kitaalamu kwa Taasisi za Umma kuhusiana na Mipango ya Rasilimali Watu;

    Divisheni ya Mafunzo

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kuandaa Sera na Miongozo inayohusu mafunzo katika Utumishi wa Umma na kuratibu utekelezaji wake.
    2. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Mafunzo katika Taasisi za Umma.
    3. Kutafuta na kuratibu upatikanaji wa fursa za Mafunzo kutoka kwa Washirika wa Maendeleo na Taasisi za Kitaaluma.
    4. Kuratibu mafunzo ya watumishi wa umma yanayodhaminiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
    5. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Mikataba ya Mafunzo kwa Watumishi wa Umma wanapokwenda masomoni
    6. Kutoa Ushauri wa kitaalamu Kwa Taasisi za Umma kuhusu utekelezaji wa Sera na Miongozo inayosimamia Mafunzo.
    7. Kuwasiliana na Mamlaka husika katika kuainisha Orodha ya Vyuo na Taasisi za kitaaluma zinazotambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
    8. Kutunza taarifa za taaluma za watumishi wa umma.

    Divisheni ya Utunzaji wa Taarifa za Watumishi Kielektroniki - (Database).

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kutunza taarifa za Watumishi wa Umma katika Mfumo wa Kielektroniki (Human Resource Management Information Systerm - Database);
    2. Kutoa msaada wa kitaalamu kwa Watumiaji wa Mfumo wa uwekaji wa taarifa za watumishi wa umma katika Taasisi za umma;
    3. Kufanya tathmini na kutoa taarifa za kiufundi katika Mfumo wa uwekaji wa taarifa za watumishi (Database)
    4. Kuweka na kuimarisha usalama katika mfumo wa uwekaji wa taarifa za watumishi wa umma;
    5. Kuhakikisha kuwa Mfumo wa kuhifadhia taarifa za Watumishi wa Umma unafanyiwa tathmini;
    6. Kushauri namna bora zaidi ya kuimarisha Mfumo wa Uwekaji wa Taarifa za Watumishi wa Umma katika Mfumo wa Kielektroniki - (Database)

    Idara ya Utawala Bora

    Majukumu ya Idara
    1. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Utawala Bora,
    2. Kutoa elimu ya Utawala Bora kupitia njia mbalimbali Kama vile vyombo vya habari, warsha, semina, makongamano na mikutano.
    3. Kuratibu masuala ya haki za Binaadamu nchini.
    4. Kujenga mashirikiano mazuri na Taasisi za utawala Bora nchini
    5. Kupokea malalamiko mbalimbali ya wananchi ili kutambua changamoto zinazowakabili wananchi.
    6. Kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya Utawala Bora nchini.

    Divisheni ya Uratibu wa Utawala Bora

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu masuala ya Utawala Bora na kuzifanyia marekebisho;
    2. Kufuatilia utekelezaji wa ripoti mbalimbali zinazotolewa na Taasisi za Utawala Bora nchini.
    3. Kufanya tathmini ya Utawala Bora nchini.
    4. Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa misingi ya Utawala Bora.
    5. Kutoa ushauri juu ya masuala ya kisera yanayohusu Utawala Bora.
    6. Kufuatilia mahusiano mazuri baina ya Sekta ya Umma, Sekta Binafsi na Wananchi.
    7. Kutoa Ushauri Kwa Taasisi juu ya utekelezaji wa masuala ya Utawala bora.
    8. Kuandaa ripot iya utekelezaji wa Divisheni na kuiwasilihas kwa Mkurugenzi.

    Divisheni ya Elimu ya Uraia

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kutoa elimu ya Uraia kwa Umma juu ya misingi ya Utawala Bora.
    2. Kuandaa na kuratibu makongamano ya Kitaifa juu ya masuala ya Utawala Bora.
    3. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa masuala mbali mbali yanayohusiana na utawala bora.
    4. Kutoa habari mbalimbali kwa jamii zinazohusu Utawala Bora.

    Divisheni ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kijamii

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kupokea na kufuatilia malalamiko na migogoro mbalimbali kutoka kwa wananchi;
    2. Kufanya uchambuzi wa malalamiko yaliyopokelewa na kutoa ushauri kwa wahusika;
    3. Kufanya usuluhishi wa migogoro inayowasilishwa na kutoa mapendekezo.
    4. Kuchukua hatua za kuzuia migogoro katika jamii;
    5. Kufanya tathmini ya malalamiko na migogoro
    6. Kuandaa ripoti ya utekelezaji wa Divisheni na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi.

    Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria

    Majukumu ya Idara
    1. Kushauri Wizara kuhusu masuala ya kisera na maendeleo ya Katiba.
    2. Kuratibu maendeleo ya Katiba na utekelezaji wake.
    3. Kushirikiana na Wizara inayohusiana na masuala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuratibu na kuandaa ripoti za haki za binaadamu.
    4. Kusajili watoaji wa msaada wa kisheria.
    5. Kuratibu, kufuatilia na kutathmini kazi za watoaji wa msaada wa kisheria.
    6. Kupokea na kupeleleza malalamiko na tabia mbaya dhidi ya watoaji wamsaada wa kisheria.
    7. Kuchukua hatua zinazofaa kuimarisha elimu ya kisheria na uwelewa wa kisheria miongoni mwa jamii na, hususan, makundi maalum kuhusu upatikanaji wa msaaada wa sheria.
    8. Kupokea na kujumuisha taarifa za mwaka za watoaji wa msaada wa kisheria.
    9. Kushajihisha na kuwezesha utatuzi wa migogoro kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro.

    Divisheni ya Kuratibu Masuala ya Katiba: -

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kushauri Wizara kuhusu masuala ya kisera na maendeleo ya Katiba;
    2. Kufatilia na kushauri kuhusu mwitikio, uimarishaji na umuhimu wa masuala ya Katiba;
    3. Kuratibu maendeleo ya Katiba na utekelezaji wake;
    4. Kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Katiba; na
    5. Kushirikiana na Wizara inayohusiana na masuala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuratibu na kuandaa ripoti za haki za binaadamu.

    Divisheni ya Usajili na Uratibu

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kusajili watoaji wa msaada wa kisheria
    2. Kupokea na kujumuisha ripoti za robo mwaka kuhusiana na huduma za msaada wa kisheria kutoka kwa watoaji wa msaada wa kisheria;
    3. Kuweka na kutunza Daftari la watoaji msaada wa kisheria.
    4. Kuweka kumbukumbu na taarifa zinazohusiana na watoaji wa msaada wa kisheria;
    5. Kuratibu, kufuatilia na kutathmini kazi za watoaji wa msaada wa kisheria; na
    6. Kupokea na kupeleleza malalamiko ya tabia mbaya dhidi ya watoaji wa msaada wa kisheria.

    Divisheni ya Elimu na Mafunzo

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kuandaa mtaala na miongozo kwa ajili ya mafunzo ya Wasaidizi wa Sheria kwa kushauriana na watoaji wa msaada wa kisheria na Taasisi za Elimu na Taasisi za Mafunzo
    2. Kusimamia na kutoa mafunzo kwa Wasaidizi wa Sheria na watoaji wengine wa huduma za msaada wa kisheria;
    3. Kubuni njia bora na za kisasa za kuendeleza programu ya elimu na mafunzo kuhusu msaada wa kisheria;
    4. Kuimarisha elimu ya sheria na uelewa wa kisheria miongoni mwa jamii na hususan, kuelimisha makundi maalumu kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria;
    5. Kuanzisha na kuendeleza programu kwa ajili ya elimu ya msaada wa kisheria na mafunzo na utoaji vyeti kwa Wasaidizi wa Sheria; na
    6. Kupokea na kujumuisha taarifa za mwaka za watoaji wa msaada wa kisheria;

    Divisheni ya Usimamizi wa Huduma za Kisheria

    Majukumu ya Divisheni
    1. Kupokea maombi na malalamiko ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria;
    2. Kuandaa na kutunza Daftari la taarifa za maombi na malalamiko kuhusu utoaji wa huduma za msaada wa kisheria;
    3. Kutayarisha taarifa mbalimbali kuhusu huduma za msaada wa kisheria na mambo mengine kwa ajili ya kuwasilishwa mbele ya Katibu Mkuu;
    4. Kumtaka mtoa msaada wa kisheria kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa mtu asiyekuwa na uwezo; na
    5. Kushajihisha na kuwezesha utatuzi wa migogoro kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro.

    Ofisi Kuu– Pemba

    Ofisi hii itakuwa na jukumu la uratibu na usimamia shughuli zote za Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kwa Pemba. Ofisi hii itaongozwa na Afisa Mdhamini ambae atateuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na anawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu. Aidha, Ofisi Kuu Pemba itakuwa na divisheni ambazo zinawakilisha utekelezaji wa majukumu mbali mbali yaliyomo katika Idara za Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

    VITENGO

    Kitengo cha Uhasibu

    Majukumu ya Kitengo
    1. Kuhakikisha usimamizi bora wa mapato yote na matumizi ya kazi za kawaida na maendeleo ya fedha za Ofisi pamoja na washirika wa maendeleo;
    2. Kufuatilia upatikanaji wa fedha kutoka Vyombo vinavyohusika;
    3. Kuhakikisha fedha zinatumika kwa mujibu wa MTEF na Mpango Kazi wa Ofisi ya Rais – Katiba na Utumishi na Utawala Bora.
    4. Kuandaa na kufanya malipo mbalimbali;
    5. Kuandaa taarifa zote za uhasibu na kuwasilisha kunakohusika kwa wakati;
    6. Kuratibu na kusimamia ‘VOTE’ zilizo chini ya Ofisi Kutoa ushauri wa kiuhasibu kuhusiana na mambo yote ya fedha; na
    7. Kusimamia rasilimali fedha, na shughuli zote za uhasibu kwa mujibu wa Sheria za Fedha pamoja na Sheria ya Ununuzi na Uondoshaji wa mali ya Umma pamoja na Kanuni zake.
    8. Kuratibu na kusimamia vyanzo vya mapato.

    Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani

    Majukumu ya Kitengo
    1. Kutoa ushauri bora kuhusiana na matumizi ya rasilimali za Ofisi;
    2. Kufanya Ukaguzi wa matumizi na mapato kwa kazi za kawaida na maendeleo (Miradi ya Ofisi);
    3. Kutoa ripoti ya awali (first draft) na ripoti ya mwisho (Final Report) ya Ukaguzi kwa Taasisi/Idara iliyokaguiwa kwa wakati;
    4. Kuratibu Vikao vya Kamati ya Ukaguzi ‘Audit Committee’;
    5. Kufanya ukaguzi wa matumizi ya rasilimali za Ofisi na kuandaa taarifa; Kufanya ukaguzi wa taratibu na mifumo ya utendaji kazi;
    6. Kufanya ufuatiliaji wa maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali;
    7. Kuandaa taarifa na kufanya ukaguzi kwa mujibu wa thamani ya fedha (Value for money).

    Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma

    Majukumu ya Kitengo
    1. Kusimamia kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma katika Taasisi ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali ya Umma isipokuwa maamuzi na utoaji wa mikataba;
    2. Kusaidia kazi za Bodi ya Zabuni;
    3. Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni;
    4. Kutoa huduma za Sekretariati ya Bodi ya Manunuzi ya Ofisi Kupanga Mpango wa Ununuzi na Mpango wa Uondoshaji wa Mali za Umma ya Ofisi;
    5. Kupendekeza taratibu za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma;
    6. Kutayarisha na kupitia vigezo vitakavyotumika kwenye Zabuni;
    7. Kutayarisha nyaraka za zabuni;
    8. Kutayarisha matangazo ya Zabuni;
    9. Kutayarisha nyaraka za mikataba na kutoa nyaraka za mikataba zilizothibitishwa;
    10. Kuziweka na kuzihifadhi taarifa na taratibu zilizotumika katika ununuzi na uondoshaji wa mali za umma;
    11. Kuunganisha shughuli za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma kwa Idara zote.
    12. Kununua, kutunza na kusimamia usambazaji wa malighafi, vifaa na huduma mbalimbali za Ofisi;
    13. Kuandaa, kutunza na kuhuisha daftari la mali mbalimbali za Ofisi;
    14. Kuandaa orodha ya vifaa katika kila ofisi.

    Kitengo cha Habari Mawasiliano na Uhusiano

    Majukumu ya Kitengo
    1. Kusimamia utayarishaji na kupitia vipeperushi na matangazo ya kuitangaza Wizara.
    2. Kusimamia uwekaji wa kumbukumbu za matukio muhimu ya Wizara.
    3. Kupiga picha za mnato na picha za video na Kutunza picha, Maktaba na marejeo.
    4. Kusimamia utayarishaji wa vipindi, Makala na vielelezo vyengine,
    5. Kusimamia uandaaji wa majarida na mabango (Posters).
    6. Kufuatilia taarifa za Taasisi katika vyombo vya habari vikiwemo mitandao ya kijamii, redio, televisheni na magazeti na kuwasilisha kwa mamlaka husika.
    7. Kupokea maoni na hoja za wananchi, kuzifuatilia na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kwa lengo la kufanyiwa kazi.
    8. Kuandika ripoti za utekelezaji wa kazi;
    9. Kupokea malalamiko kutoka kwa wadau na Kufuatilia maendeleo na changamoto za mahusiano ya Wizara.
    10. Kuweka mazingira mazuri na kukuza mahusiano kazini baina ya watumishi wa Ofisi, watumishi wa Taasisi nyengine na jamii kwa ujumla (afya, michezo, usalama na utamaduni);
    11. Kuratibu na kusimamia masuala mbalimbali ya kiitifaki ya Ofisi na Kuratibu na kupokea wageni wa Wizara
    12. Kuhakikisha kuwa Habari zinazotolewa zimehakikiwa au kuhaririwa vyema.

    Kitengo cha Sheria

    Majukumu ya Kitengo
    1. Kutoa ushauri na msaada wa masuala ya kisheria katika Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
    2. Kutoa tafsiri za Sheria, Kanuni, Miongozo na mikataba mbalimbali kwa Ofisi, Idara/Taasisi na vitengo vya Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora;
    3. Kuweka na kuhifadhi Kumbukumbu na majalada ya kesi za madai zinazohusiana na Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora;
    4. Kutoa msaada wa kitaalamu wakati wa maandalizi au uhuishaji wa rasimu mbalimbali za kisheria na kuwasilisha rasimu hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Wizara inayohusiana na masuala ya Sheria kwa hatua zaidi;
    5. Kushiriki majadiliano mbalimbali yanayohusu sekta kuingia katika makubaliano au mikataba maalumu ya Ofisi/kisekta;
    6. Kutunza na kuhifadhi nyaraka zote za kisheria na mikataba inayohusu majukumu ya Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
    7. Kuchambua na kutafsiri sheria za sekta na kutoa ushauri wa kisheria;
    8. Kupitia na kupendekeza marekebisho ya sheria za zinazohusiana na Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

    Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

    Majukumu ya Kitengo
    1. Kusimamia muundo na mpangilio ya Sheria na taratibu katika kuendeleza na kutumia mfumo wa mawasiliano ya habari
    2. Kufanya uchambuzi na kubuni mifumo ya kiteknolojia, habari na mawasiliano ya kusaidia Ofisi kuweza kutoa huduma na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu;
    3. Kuandaa na kutekeleza mkakati wa kiteknolojia, habari na mawasiliano pamoja na kufanya tathmini;
    4. Kufanya ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa Sera ya teknolojia, habari na mawasiliano;
    5. Kuhakikisha mipango ya uanzishwaji na uendelezaji wa teknolojia ya mawasiliano ipo katika hali nzuri na yenye gharama nafuu;
    6. Kutunza, kutoa ushauri na kuratibu ununuaji wa vifaa (hardware) vya kiteknolojia, habari na mawasiliano pamoja na programu (software);
    7. Kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi bora ya mfumo wa mawasiliano ya habari (hardware & software);
    8. Kuanzisha, kuratibu na kuelekeza matumizi ya barua pepe;
    9. Kuanzisha na kuwezesha matumizi ya mtandao kiambo ‘Local Area Network (LAN)’ na mtandao mpana ‘Wide Area Network (WAN)’;
    10. Kuandaa na kutunza ‘web-portal’ na mtandao wa Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora;
    11. Kutengeneza na kuhakikisha matumizi salama ya mfumo na vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano;
    12. Kutayarisha njia ya utaratibu mzuri wa kuboresha utendaji na utoaji wa huduma na utekelezaji kazi za Ofisi kupitia mfumo wa teknolojia ya habari na mawasiliano;
    13. Kutoa mafunzo kwa watumishi juu ya utumiaji wa mifumo na vifaa vya kiteknolojia, habari na mawasiliano;
    14. Kuratibu maendeleo ya uhifadhi wa program katika kuhakikisha usalama wa taarifa;
    15. Kufanya tathmini ya utekelezaji wa mfumo wa habari na mawasiliano katika Ofisi;
    16. Kutunza Kumbukumbu za mfumo wa matumizi ya Kompyuta.