Muundo wa Wizara
OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA UTUMISHI NA UTAWALA BORA.
Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora utaongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora na Katika ngazi ya utendaji Muundo utaongozwa na Katibu Mkuu akisaidiwa na Naibu Katibu Mkuu.
Aidha, Katibu Mkuu anaesimamia Idara Sita (6), Ofisi moja (1) ya Afisa Mdhamini Pemba na Vitengo sita (6) vinavyoripoti moja kwa moja kwa Katibu Mkuu. Aidha, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora ina jumla ya Taasisi Kumi na sita (16) zinazojitegemea, mchanganuo wa Idara, Ofisi, vitengo na Taasisi Zinazojitegemea ni kama ifuatavyo: -
Idara na Ofisi
- Idara ya Uendeshaji na Utumisihi;
- Idara ya Mipango, Sera na Utafiti;
- Idara ya Miundo ya Taasisi, Utumishi na Maslahi ya Watumishi.
- Idara ya Utawala Bora;
- Idara ya Maendeleo ya Rasilimali watu.
- Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria;
- Ofisi ya Mdhamini – Pemba.
VitengoVinavyojitegemea
- Kitengo cha Fedha na Uhasibu;
- Kitengo cha Manunuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma;
- Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani;
- Kitengo cha Sheria;
- Kitengo cha Uhusiano; na
- Kitengo cha Teknolojia Habari, Elimu na Mawasiliano
MUUNDO WA WIZARA
Maelezo ya Muundo wa Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora ni kama ifuatavyo: -
WAZIRI
Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora anateuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa chini ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu 42 (2), Waziri ana majukumu ya kuratibu na kusimamia shughuli zote zinazotekelezwa na Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
KATIBU MKUU
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora anateuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa chini ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu Namba.50 (2) na (3) akiwa ndie msimamizi na Mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku za Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
NAIBU KATIBU MKUU
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora nae pia anateuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uwezo aliopewa chini ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Namba. 50 (3) akiwa ndie Msaidizi Mkuu wa Katibu Mkuu katika utekelezaji wa shughuli za kila siku za Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
IDARA NA OFISI
Muundo una jumla ya Idara saba (7) na Ofisi moja (1) ufafanuzi wa Idara na Ofisi hizo ni kama ifuatavyo:
Idara ya Uendeshaji na Utumishi
Idara hii inahusika na utoaji wa huduma za uendeshaji na utumishi, kusimamia maslahi ya rasilimali watu, pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Ofisi. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Idara ya Uendeshaji na Utumishi inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni Divisheni ya Uendeshaji, Divisheni ya Utumishi na Divisheni ya Utunzaji wa Kumbukumbu
Divisheni ya Uendeshaji
Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Ofisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Utumishi
Divisheni hii itahusika na masuala ya maendeleo na usimamizi wa rasilimali watu ndani Ofisi ikiwemo ajira, mishahara, mafunzo kwa watumishi, upimaji utendaji kazi, upandishaji vyeo. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu
Divisheni hii itahusika na shughuli za uwekaji wa kumbukumbu na uhifadhi wa nyaraka na kazi mbali mbali za Ofisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Idara ya Mipango Sera na Utafiti
Idara hii inashughulikia na uandaaji wa mipango ya Ofisi, bajeti, ufuatiliaji na tathmini ya programu na miradi, kutayarisha na kuzifanyia mapitio Sera na kufanya tafiti za Ofisi. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Idara inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni Divisheni ya Ufuatiliaji na Tathmini, Divisheni ya Maendeleo ya Sera na Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo
Divisheni ya Ufuatiliaji Utafiti na Tathmini
Divisheni hii itahusika na shughuli za ufatiliaji na ufanyaji wa tathimini wa mipango mbali mbali ya Ofisi iliyopangwa kutekelezwa. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Maendeleo ya Sera
Divisheni hii itahusika na shughuli za uandaaji na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera mbalimbali zinazoandaliwa na Ofisi ili kuhakikisha zinakwenda sambamba na malengo yaliyokusudiwa. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Mipango ya Kisekta na Maendeleo
Divisheni hii itahusika na shughuli za ukusanyaji wa taarifa na kutayarisha Mipango ya kisekta, kuandaa bajeti, kutayarisha taarifa ya utekelezaji. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Idara ya Miundo na Maslahi ya Watumishi.
Idara hii itahusika na majukumu kuandaa miongozo na matoleo mbalimbali yanayohusu masuala ya utumishi, kupendekeza kuhusiana na Miundo ya Taasisi, Mishahara, Maposho na Maslahi mengineo ya watumishi na ushughulikiaji wa Malalamiko mbali mbali. Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Idara inaundwa na Divisheni nne (4) ambazo ni Divisheni ya Uchambuzi Kazi wa Miundo, Divisheni ya Maslahi ya Watumishi, Divisheni ya Matoleo na Miongozo na Divisheni ya Ushughulikiaji wa Malalamiko.
Divisheni ya Uchambuzi Kazi Miundo na Mifumo
Divisheni hii itahusika na shughuli za kutayarishaMiundo ya Utumishi, mishahara na Miundo ya Taasisi pamoja na pamoja na mifumo mengine ya malipo. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Maslahi ya Watumishi
Divisheni hii itahusika na usimamizi wa Maslahi ya Watumishi, ikijumuisha za Mishahara, Maposho na stahiki nyengine za malipo katika utumishi wa Umma Zanzibar. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Matoleo na Miongozo
Divisheni hii itahusika na shughuli za kutayarisha Kuandaa, kutoa Miongozo na Matoleo mbalimbali yanayohusu masuala ya Kiutumishi Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Utumishi wa Umma. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Ushughulikiaji wa Malalamiko na Ushauri
Divisheni hii inahusika na Kushughulikia Malalamiko ya Watumishi wa umma. Malalamiko ambayo yanayohusiana na Masuala ya kiutumishi katika Utumishi wa Umma Zanzibar ya kijumuisha Stahiki za Mishahara Posho na mfano wa hayo.
Idara ya Mipango ya Rasilimali Watu
Idara hii itahusika na majukumu ya uandaaji wa Sera na Miongozo inayohusu mipango ya rasilimali watu, kusimamia matumizi bora ya rasilimali watu katika Taasisi za Umma na utoaji wa vibali vya ajira. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Idara inaundwa na Divisheni tatu (3) ambazo ni Divisheni ya Mipango ya Rasilimali Watu Divisheni ya Mafunzo na Divisheni Utunzaji wa Taarifa za Watumishi kwa njia ya Kielektroniki.
Divisheni ya Mipango ya Rasilimali Watu
Divisheni hii itahusika na shughuli za uandaaji wa Sera na Miongozo inayohusu Mipango ya Rasilimali Watu pamoja na kusimamia utekelezaji wake. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Mafunzo
Divisheni hii itahusika na uandaaji wa Sera na Miongozo inayohusu mafunzo uratibu wa upatikanaji wa fursa za Mafunzo kwa watumishi wa umma. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Utunzaji wa Taarifa za Watumishi Kielektroniki - (Database).
Divisheni hii itahusika na shughuli za utunzaji wa taarifa za Watumishi wa Umma katika Mfumo wa Kielektroniki, Kutoa msaada wa kitaalamu kwa Watumiaji wa Mfumo wa uwekaji wa taarifa za watumishi wa umma. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Idara ya Utawala Bora
Idara hii itahusika na majukumu ya uratibu na usimamizi wa utekelezaji wa sera ya utawala bora, kutoa elimu ya utawala bora na kuratibu masuala ya haki za Binaadamu nchini. Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Idara ya Utawala Bora imeundwa Divisheni (3) ambazo ni Divisheni ya Uratibu wa Utawala Bora Divisheni ya Elimu ya Uraia na Divisheni ya Usuluhishi wa Migogoro.
Divisheni ya Uratibu wa Utawala Bora
Divisheni hii itahusika na usimamizi wa utekelezaji wa sheria zinazohusu masuala ya utawala bora, kufanya ufatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa ripoti zinazohusiana na utawala bora nchini. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Elimu ya Uraia
Divisheni hii itahusika nautoaji wa elimu ya uraia kwa wananchi juu ya misingi ya utawala bora, kuandaa na kuratibu makongamano ya ya masuala ya utawala bora. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Divisheni ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kijamii
Divisheni hii itahusika upokeaji na ufuatiliaji wa malalamiko na migogoro mbalimbali kutoka kwa wananchi, kutoa ushauri na mapendekezo juu ya kuchukua hatua za mbali mbali za usuluhishi wa migogoro katika jamii. Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria
Idara hii itahusika na majukumu ya utoaji wa miongozo ya kisera kwa watoaji wa msaada wa kisheria, kufanya usajili wa watoaji wa msaada wa kisheria na kuratibu, kufuatilia na kutathmini kazi za watoaji wa msaada wa kisheria na kutoa maelekezo ya jumla kwa ajili ya utekelezaji uanofaa wa programu za msaada wa kisheria. Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Idara itakuwa na divisheni 4 ambazo ni Divisheni ya Kuratibu Masuala ya Katiba, Divisheni ya Usajili na Uratibu, Divisheni ya Elimu na mafunzo na Divisheni ya Usimamizi wa huduma za kisheria.
Divisheni ya Kuratibu Masuala ya Katiba
Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni na itakuwa na jukumu la kuratibu kufuatilia na kushauri masuala ya Katiba kama ifuatavyo.
Divisheni ya Usajili na Uratibu
Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni na itakuwa na jukumu la
ufuatiliaji na tathmini kwa watoaji wa huduma za msaada wa kisheria.
Divisheni ya Elimu na Mafunzo
Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni na itakuwa na jukumu la utoaji wa elimu kuhusu msaada wa kisheria pamoja na kutoa mafunzo kwa watoaji wa huduma za msaada wa kisheria.
Divisheni ya Usimamizi wa Huduma za Kisheria
Divisheni hii itaongozwa na Mkuu wa Divisheni na itakuwa na jukumu la kusimamia huduma za kisheria katika masuala ya migogoro inayohusiana na utoaji wa huduma za msaada wa kisheria.
Ofisi Kuu– Pemba
Ofisi hii itakuwa na jukumu la uratibu na usimamia shughuli zote za Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kwa Pemba. Ofisi hii itaongozwa na Afisa Mdhamini ambae atateuliwa wa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na anawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu.
Aidha, Ofisi Kuu Pemba itakuwa na divisheni ambazo zinawakilisha utekelezaji wa majukumu mbali mbali yaliyomo katika Idara za Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.
VITENGO
Muundo una Vitengo sita (6) vilivyo chini ya Katibu Mkuu vitengo hivyo ni kama vifuatavyo: -
Kitengo cha Uhasibu
Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya utayarishaji na ufanyaji malipo mbali mbali ndani ya Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora. Kitengo hiki kitaongozwa na Mhasibu Mkuu.
Kitengo cha Ukaguzi wa Hesabu za Ndani
Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya ushauri na udhibiti wa mali na fedha za Ofisi, Kufanya ukaguzi wa matumizi ya rasilimali za Ofisi. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani.
Kitengo cha Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma
Kitengo hiki kitahusika na kutoa huduma za ununuzi na na usimamizi wa uondoshaji wa mali za umma ndani ya Ofisi. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.
Kitengo cha Habari Mawasiliano na Uhusiano
Kitengo hiki kitahusika na Masuala ya Habari Mawasiliano na Uhusiano kati ya Ofisi na taasisi nyengine, kuratibu malalamiko na kuzitangaza shughuli za Ofisi. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.
Kitengo cha Sheria
Kitengo hiki kitahusika na kutoa huduma za ushauri wa masuala ya kisheria katika Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo.
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kitengo hiki kitahusika na majukumu ya kutoa huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano ndani Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora. Kitengo hiki kitaongozwa na Mkuu wa Kitengo
Organization Structure.