Ujumbe wa Waziri
Mh. Waziri Haroun Ali Suleiman
Kama tunavyoelewa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawajali sana wananchi wake hasa katika kuhakiksiha
kuwa inazungukwa na jamii yenye ustawi mzuri uliomarika katika kila nyanja ya maisha pamoja na kuhakikisha
wananchi wake hususan wanyonge na wasiojiwezawanapatiwa msaada wa kisheria bila ya usumbufu wowote.
Hivyo, lengo kuu la Wiki ya Msaada wa Kisheria ni kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa jamii yetu inayotuzunguka. Kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya msaada wa
Kisheria kwa mwaka 2023 ni “MAZINGIRA WEZESHI KWA WATOA MSAADA WA KISHERIA NI DARAJA LA UPATIKANAJI HAKI”.
Kauli mbiu hii ina lengo la kuhakikisha kunakuwepo na mazingira mazuri ya utoaji msaada wa kisheria kwa
watoaji wa msaada wa kisheria. Bado kuna changamoto kubwa kwa watoaji wa msaada wa kisheria ikiwemo uhaba wa bajeti na upatikanaji wa
Ofisi za kudumu zenye mazingira mazuri ya utoaji wa msaada wa kisheria.
Aidha, ifahamike kuwa watoaji wa msaada wa kisheria hufanya kazi zao kwa kujitolea, uzalendo na jitahada
kubwa katika kuhakikisha wananchi wasio na uwezo, watu wenye ulemavu na watu wa makundi maalum
wanapatiwa msaada wa kisheria hivyo, kufanikiwa kwa jitahada zao inategemea na uwepo na mazingira
wezeshi ikiwemo mashirikiano kwa jamii, upatikanaji wa rasilimali fedha za kutosha, vitendea kazi na kadhalika.
Ni matarajio yetu kwa kauli mbiu hii kuwa ni chachu ya upatikanaji wa mazingira mazuri kwa watoaji wa msaada
wa kisheria.