TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA NA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

Posted: 2019-08-28 14:26:38
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi ya kazi ya Fundi Sanifu Madawa daraja la III katika Wizara ya Afya kwa ajili ya Wilaya mbali mbali za Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

UNGUJA
JINA LA WILAYA IDADI
1 Wilaya ya Kati 17
2 Wilaya ya Kaskazini “A” 8
3 Wilaya ya Kaskazini “B” 11
4 Wilaya ya Kusini 6
5 Wilaya ya Mjini 14
6 Wilaya ya Magharibi “A” 3
7 Wilaya ya Magharibi “B” 9
PEMBA
1 Wilaya ya Chake Chake 10
2 Wilaya ya Micheweni 13
3 Wilaya ya Mkoani 13
4 Wilaya ya Wete 16

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ‘Ufamasia’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


Aidha, Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kama ifuatavyo:-

1. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1”
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Kutunza Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 04 Septemba, 2019 wakati wa saa za kazi.

Close
Close