TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI

Posted: 2023-03-14 15:12:11
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar kwa kada mbali mbali kama ifuatavyo:
1.Afisa uvuvi daraja la II (ZPSF-02) nafasi 2 Pemba
Sifa za waombaji
1.Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka arubaini na sita (46).
2.Awe amehitimu Shahada ya kwanza ya Uvuvi au fani nyengine ya masuala ya uvuvi au inayolingana nayo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu:
1.Kukusanya na kutayarisha Takwimu katika sekta ya Uvuvi.
2.Kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya wavuvi.
3.Kufanya ukaguzi wa ubora wa utayarishaji wa mabwawa ya samaki na ufugaji.
4.Kusimamia uzalishaji (breeding)/ufugaji wa samaki bora.
5.Kukusanya na kutayarisha Takwimu za mazao ya baharini.
6.Kushajiisha na kuratibu uwekezaji wa uhifadhi wa baharini katika ngazi ya Wilaya/Mkoa.
7.Kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya jamii katika uhifadhi wa maeneo ya baharini.
8.Kuwaelimisha wananchi juu matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
9.Kufanya ukaguzi katika maeneo ya uhifadhi bahari ili kudhibiti matumizi haramu katika maeneo ya hifadhi.
10.Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
11.Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
2.Afisa uvuvi msaidizi daraja la III (ZPSD-03) nafasi 1 Pemba
Sifa za waombaji
1.Awe Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka arubaini na sita (46).
2.Awe amehitimu Stashahada ya Kawaida (Ordinary Diploma) ya Uvuvi au fani inayolingana nayo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Majukumu:
1.Kushiriki katika kuweka Takwimu za Uvuvi wa samaki pamoja na mazao mengine ya baharini
2.Kuthibitisha ya kwamba zana za Uvuvi zinazotumiwa zinafuata Viwango vilivyowekwa.
3.Kuwashajihisha wananchi hasa wa vijijini katika ujenzi wa mabwawa na ufugaji wa samaki.
4.Kuandaa ripoti za utekelezaji wa kazi ikiwemo ripoti ya robo, nusu na mwaka.
5.Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na Mkuu wake.
Jinsi ya kuomba:
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa maombi ya ajira (Zanajira) kupitia anuani ifuatayo:- http://portal.zanajira.go.tz kuanzia tarehe 14 Machi, 2023 hadi tarehe 28 Machi, 2023.
Mfumo huo pia unapatikana katika tovuti ya Tume ya Utumishi Serikalini www.zanajira.go.tz.
Maombi yote yatumwe kwa anuani fuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S.L.P 1587,
ZANZIBAR
Muombaji anatakiwa kuanisha nafasi ya kazi aliyoomba.

Kwa msaada wa kitaalamu wasiliana na Tume ya Utumishi Serikalini kupitia email: helpdesk@zanajira.go.tz au simu Nam. 0773 101012.

AHSANTENI.
Close
Close