Waziri Haroun Azungumza na Ujumbe kutoka Oman

news phpto

Picha kwa hisani ya Kitengo cha Habari

Oman imeahidi kuendeleza program mbali mbali zinazohusiana na maswala ya kiislam kwa kushirikiana na ofisi ya Mufti wa Zanzibar.

Tamko hilo limetolewa na Balozi mdogo wa Oman aliekuepo Zanzibar Nd. Said Salim Hemed Alsinawi wakati timu hiyo ya wataalamu ilipofanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman ofisini kwake Mazizin Zanzibar.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa makubalianao ya viongozi wa Oman na Zanzibar wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alipofanya ziara nchini Oman hivi karibuni.

Ametaja maeneo ambayo yatapewa kipaumbele kwa mafunzo hayo kwa vijana wa Zanzibar juu ya maadili ya kiislam, zakka na hijja ili kuwajengea uwezo zaidi.

Waziri Haroun ameelezea ziara ya wataalamu hao kuwa ni hatua ya awali na hatimae vijana wa Zanzibar watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo nchi Oman ambapo mafunzo hayo yanaendelea kutolewa masjid jamii zinjibar Mazizini Zanzibar

Close
Close