Wiki ya Sheri Kinuni
Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kuwatafutia watoto vyeti vya kuzaliwa mara tuu baada ya kuzaliwa ili kuepusha matatizo yanayojitokeza hususan wanapohitaji huduma za kijamii.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Sheria kutoka Idara ya Msaada wa kisheria Zanzibar Nd. Salma Suleiman Abdulla wakati akitoa elimu ya umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa kwa wajasiria mali katika Shehia ya Mchikichini Wilaya ya Mgharibi A.
Amesema endapo suala la vyeti vya kuzaliwa litawekewa umuhimu na kutiliwa mkazo matatizo madogo madogo kama vile vikwazo wanavovipata wakati wa kujiandikisha skuli,utafutaji wa ajira na pasi ya kusafiria yanaweza kuondoka.
Amebainisha kuwa kunafaida kubwa ya kusajili vyeti mara baada ya watoto kuzaliwa ikwemo kuepuka gharama kubwa na faini watakayo toleshwa pamoja na kunusuru muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo.
Msaidizi wa Sheria wa Wilaya hiyo Nd. Mwaka Mzee amewasisitiza wanafamilia kuacha tabia ya kufunga ndoa kiholela nakuzisajili kisheria pale wanapooana ili kuepuka mizozo hususan wakati wa masuala ya urithi.
Katibu wa Shehia Mchikichini Nd. Zuhura Said Khamis amewaasa wanafamilia hao kuwana utaratibu wa kujifungulia Hospitali ili serikali iweze kupata takwimu sahihi za watoto wanao zaliwa na kuwa na urahisi wa kupata vyeti vya kuzaliwa.
Maafisa wa sheria wakiambatana na wasaidizi wa sheria wamekua katika muendelezo wa kutoa taaluma kwa umma katika shehia mbali mbali ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya wiki ya sheria kitaifa inayofikia kilele chake tarehe 13 mwezi huu.