WaziriHaroun Ali Suleiman awataka wafanyakazi (ZAECA)kujiamini

news phpto

kutoka kitengo cha habari

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amewataka wafanyakazi wa Mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi(ZAECA)kujiamini wakati wanapotekeleza majukumu yao,muhimu kuzingatia misingi ya kazi na kufuata sheria wakati wanapotekeleza kazi zao.

Hayo ameyaeleza wakati alipotembelea na kukutana na uongozi na wafanyakazi huko ofisini kwao kilimani Mjini Zanzibar .

Alisema endapo watajiamini na kuonesha uaminifu heshima na maadili ya kazi na utendaji wao utaweza kuwa imara na kuwa na nguvu ya kuweza kujitegemea.

WazirI Haroun alisema wanaochukua hukumu ni vyema kuchukua hatua za kidiplomasia ili kuweza kwenda sambamba na sheria bila ya kuvuka misingi na maadili ya kazi waliopangiwa.

Hakusita kuzungumzia suala la kuzidisha mashirikiano katika kazi kati ZAECA ,DPP na Jeshi la polisi Tanzania ili kuweza kuleta ufanisi mzuri wa kazi bila ya kuwepo malalamiko yoyote.

Akizungumzia suala stahiki za wafanyakazi wa chini amesema hicho ni kilio cha wafanyakazi wengi ila ameahidi kulifanyia kazi tatizo hilo.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa ZAECA Nd.Ali Abdalla Ali amesema Mamlaka ilifanikiwa kuokoa jumlaya shilingi za kitanzania Bilioni Sita Milioni Mia Tatu Themanini na Tisa laki tatu Tisiini na nne elfu mia na ishirini na nne(6,389,394,824/=) na kwa upande wa udhibiti mamlaka ilifanikiwa kuokoa na kurejesha serikalini ,jumla ya shilingi za kitanzania Bilioni moja Milioni mia mbili na hamsini na laki sita kumi na tisa elfu mia tatu na sitini na tano(1,252,619,365/=)na kwa upande wa urejeshaji mali,mamlaka ilifanikiwa kuokoa jumla ya shilingi za kitanzania Bilioni tano milioni mia moja thelasini na sita laki saba sabiini na tano elfu mia nne na hamsini na nane (5,136775458/=)fedha hizo zote ziligawanyika katika makundi mawili tofauti.

Aidha ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukuza uwelewa kwa wananchi kwa kutoa elimu na kuripoti taarifa za vitendo vya rushwa vinavyotokea katika jamii .

Nao baadhi ya wafanyakazi wakichangia wamesema wanakabiliwa na changamoto ya fedha za operation ili kuweza kutengeneza majukumu yao kwa ufanisi na tija kwa ujumla.

Aidha Makamanda wa Wilaya wameomba kupatiwa Ofisi za uhakika na usalama pamoja na kupatiwa usafiri ambao utakao weza kuwarahisishia nakufika sehemu mapema, kuepusha usumbufu utakao jitokeza katika utendaji wao wa kazi.

Close
Close