SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Kumtunuku Shahada ya uzamivu ya Heshima, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utawala Bora, Mwalimu haroun Ali Suleiman Chuo cha Taifa cha Zanzibar

Mwalimu Haroun alianza kazi mwaka 1976 akiwa mwajiriwa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na akiwa Mwakilishi katika jimbo la Makunduzi kuanzia mwaka 2000 hadi sasa. Dk. Haroun anatajwa kuwa ni miongoni mwa magwiji wenye uzoefu kwenye utumishi wa umma, heshima ya kujituma na pia kuweka historia kubwa ya kupewa heshima ya kishika nyadhifa mbali mbali za uongozi kwa miaka 25 mfululizo katika awamu tano tafauti. Pamoja kuitumikia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzia mwaka 1976 akiwa mwalimu wa skuli hadi mwaka 1992 bila kusita. Skuli alizowahi kufundisha ni Skuli ya Makunduchi (1976), Skuli ya Sekondari ya Benbella (1978), na Skuli ya Haile Sellasie (1979) ambapo wmaka 1985 alishika wadhifa wa Mwalimu Mkuu hadi mwaka 1992.