info@utumishismz.go.tz +255 777 123456

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

UTANGULIZI

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliunda upya Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora mnamo mwezi wa April, mwaka 2019 ikiwa kwa ajili ya kusimamia, kuimarisha na kukuza masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar. Mara baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya 8 kuingia madarakani mnamo tarehe 5 Novemba 2020 hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa majukumu ya Serikali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025 na Dira ya Maendeleo ya 2050. Miongoni mwa hatua hizo zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kwa madhumuni ya Kuwa na Jamii inayoheshimu Misingi ya Utumishi, Haki, Usawa,Sheria, na Utawala Bora kwa Kuimarisha maendeleo ya Utumishi wa Umma, Kuweka Misingi ya Usawa, Sheria, upatikanaji wa Haki, kwa kuzingatia Utawala Bora ili kuweza kufikia lengo la Kuimarisha utendaji kazi katika Utumishi wa umma, kuratibu masuala ya Katiba, Sheria, na Utawala Bora na mahusiano ya kikanda na kimataifa.