SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Tendeni mema ili mutajwa kwa wema ndani ya jamii.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kutenda mema ili kutajwa kwa wema ndani ya jamii pale wanapotangulia mbele ya haki. Hayo ameyasema leo, tarehe 16 Januari 2026, alipokuwa akijumuika na waumini katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti wa Bamita Chumbuni, Mkoa wa Mjini Magharibi. Katika swala hiyo ya Ijumaa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman, pia amehudhuria, akionyesha mshikamano wa viongozi wa serikali na jamii ya kidini katika kutimiza malengo ya maendeleo na heshima ya kila mmoja.Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kote, hatua inayolenga kuhakikisha matarajio makubwa ya wananchi yanatimizwa, na kuwa kila mmoja ana nafasi ya kushirikiana katika kujenga taifa lenye maendeleo endelevu.Historia ya Msikiti wa BAMITA ni ya kipekee, kwani uliwekewa jiwe la msingi na Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi mwaka 1981, na tangu wakati huo umekuwa kitovu cha ibada na mshikamano wa waumini.Alhaj Dkt. Mwinyi anaendelea na utaratibu wake wa kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa, akitembelea misikiti mbalimbali mijini na vijijini, hatua inayothibitisha uhusiano wa karibu kati ya viongozi wa kisiasa na jamii ya kidini, huku akiendelea kuhimiza maadili mema na mshikamano wa kijamii