SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

OFISI YA RAIS KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA

Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman ashiriki katika ufunguzi wa Viwanja vya Michezo Gombani, Kisiwa cha Pemba.”

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman ameshiriki katika hafla ya ufunguzi wa Viwanja vya Michezo Gombani, vilivyopo Kisiwa cha Pemba. Ufunguzi wa viwanja hivyo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo na kuwapatia vijana mazingira bora ya kukuza vipaji vyao. Hatua hii inaakisi dhamira ya Serikali ya kuimarisha utawala bora kwa kuwekeza katika miundombinu ya kijamii inayochochea ushirikishwaji wa wananchi, hususan vijana, katika shughuli za maendeleo.